Na Mwandishi, Jeshi la Polisi- Arusha.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kupitia klabu yake inayofaya mazoezi ya kukimbia (Joggin) kila siku ya Jumamosi imekadhiwa jumla ya jezi 200 na benki ya CRDB kanda ya kaskazini kwa ajili ya kuimarisha mazuri katika kukabiliana na uhalifu.
Akipokea Jezi hizo Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Peter Lusesa amesema kuwa Jeshi hilo kwa kushirikiana na wananchi hukimbia mbio fupi kila siku ya jumamosi ambapo ameishukuruku benki hiyo kwa kutoa Jezi kwa klabu hiyo.
ACP Lusesa ameongeza kuwa michezo husaidia kuwaleta watu karibu na Jeshi la Polisi ambapo inasaidia kubadilishana taarifa za kihalifu na wahalifu kw a sababu wananchi wanaondoa hofu ya kukutana na Polisi.
Katika hatua nyingine ACP Lusesa amewaomba wananchi kuendelea kujiunga na Polisi Jogging club ili kufanya mazoezi kwa Pamoja ambayo yanasidia kuepuka magonjwa nyemelezi ambayo tiba yake ni mazoezi.
Kwa upande wake Meneja wa Crdb kanda ya Kaskazini Bw. Cosmas Sadati amesema ili biashara iweze kufanyika vizuri inahitaji usalama wa kutosha, hivyo wakaona ni vyema kuungana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kwa kutoa Jezi kwa ajili ya klabu hiyo ya Polisi ambayo inawaunganisha wananchi Pamoja na wadau mbalimbali.
Koplo wa Jeshi la Polisi Sheilla Mwakaleja Pamoja na kushukuru benki hiyo kwa vifaa hivyo,amebainisha kuwa vifaa hivyo vitaifanya klabu hiyo kuwa na muonekano mzuri unaofanana wakati wakifanya mazoezi barabarani.
Nae Mkaguzi kata ya Sekei Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/INSP Ditrick Mtuka ambaye ni miongioni wa askari walio anzisha klabu hiyo amewaomba wakazi wa kata hiyo kujiunga na klabu hiyo ya ili kujenga umoja na kubadilishana taarifa za uhalifu na wahalifu.
Nae Bwana Adeni Sinkala amebainisha kuwa Jezzi hizo zitaongeza hali na motisha katika klabu hiyo huku akiwaomba wadau wengine kushiriki lakini pia kuiga mfano wa CRDB Bank.