Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Watumishi Housing Investment (WHI) Dkt. Fred Msemwa (kulia) wakipongezana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Shadong Hi- Speed Group nchini Tanzania Bw. Li Manchao leo Julai 29, 2024, Dar es Salaam baada ya kutia saini ya makubaliano ya utekeleza wa mradi wa Nyumba 101 zenye thamani ya shilling bilioni 18.6 zinazotarajiwa kujengwa Mikocheni Regent Estate, Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Watumishi Housing Investment (WHI) Dkt. Fred Msemwa akizungumza jambo leo Julai 29, 2024 Dar es Salaam katika hafla fupi ya utiaji saini na Mkandarasi kutoka Kampuni ya Shadong Hi- Speed Group kwa ajili ya utekeleza wa mradi wa Nyumba 101 zenye thamani ya shilling bilioni 18.6 zinazotarajiwa kujengwa Mikocheni Regent Estate, Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Ushauri na Ubunifu – WHI Arch. Sephania Solomon akizungumza jambo leo Julai 29, 2024, Dar es Salaam katika hafla fupi ya utiaji saini na Mkandarasi kutoka Kampuni ya Shadong Hi- Speed Group kwa ajili ya utekeleza wa mradi wa Nyumba 101 zenye thamani ya shilling bilioni 18.6 zinazotarajiwa kujengwa Mikocheni Regent Estate, Dar es Salaam.
Meneja wa Biashara Kampuni ya Shadong Hi- Speed Group Bw. Meng Lingyang akizungumza jambo leo Julai 29, 2024, Dar es Salaam katika hafla fupi ya utiaji saini na Taasisi ya Watumishi Housing Investment (WHI) kwa ajili ya utekeleza wa mradi wa Nyumba 101 zenye thamani ya shilling bilioni 18.6 zinazotarajiwa kujengwa Mikocheni Regent Estate, Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Sheria Taasisi ya Watumishi Housing Investment (WHI) Mwanasheria Joel Maeda (katikati) akimuelekeza jambo Mkurugenzi wa Kampuni ya Shadong Hi- Speed Group nchini Tanzania Bw. Li Manchao katika hafla fupi ya utiaji saini na Mkandarasi wa Kampuni hiyo kwa ajili ya utekeleza wa mradi wa Nyumba 101 zenye thamani ya shilling bilioni 18.6 zinazotarajiwa kujengwa Mikocheni Regent Estate, Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Watumishi Housing Investment (WHI) Dkt. Fred Msemwa (kulia) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Shadong Hi- Speed Group nchini Tanzania Bw. Li Manchao wakiwa katika picha ya pamoja leo Julai 29, 2024, Dar es Salaam wakati wakitia saini ya makubaliano ya utekeleza wa mradi wa Nyumba 101 zenye thamani ya shilling bilioni 18.6 zinazotarajiwa kujengwa Mikocheni Regent Estate, Dar es Salaam.
……..
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Taasisi ya Watumishi Housing Investment (WHI) imeingia makubaliano na Mkandarasi kutoka Kampuni ya Shadong Hi- Speed Group kwa ajili ya kutekeleza wa mradi wa Nyumba 101 zenye thamani ya shilling bilioni 18.6 zinazotarajiwa kujengwa Mikocheni Regent Estate, Dar es Salaam jambo ambalo litawasaidia watumishi wa umma kumiliki makazi bora kwa gharama nafuu.
Akizungumza leo Julai 29, 2024 jijini Dar es Salaam katika hafla fupi ya utiaji saini na Mkandarasi kutoka Kampuni ya Shadong Hi- Speed Group, Mkurugenzi Mtendaji wa WHI Dkt. Fred Msemwa, amesema kuwa ujenzi wa nyumba hizo unatarajia kuanza mwezi Agosti mwaka huu na unatarajia kukamilika baada ya miezi 18.
Dkt. Msemwa amesema kuwa nyumba hizo zitauzwa kwa kufata utaratibu maalum wa unafuu kwa watumishi wa umma, huku akieleza kuwa nyumba 218 zitajengwa katika Mikoa ya Dodoma, Lindi, Mtwara, Singida, Pwani, Ruvuma katika mwaka wa fedha 2024/2024.
Amesema kuwa katika kufanisha ujenzi wa mradi huo watashirikiana na kampuni ya kizalendo katika kusimamia ili kuhakikisha wanapata uzoefu kutoka kampuni ya kichina.
“Bei ya nyumba ya chumba kimoja yenye sebule, chumba cha kulala, choo, stoo, jiko, balcony itaanzia shilling milioni 99 na bei ya vyumba vitatu vya kulala, sebule, stoo, balcony itaanzia milioni 234” amesema Dkt. Msemwa.
Dkt. Msemwa amesema kuwa bei za nyumba hizo ni nafuu ukilinganisha na nyumba nyengine katika eneo la mikocheni huku akibainisha kuwa utaratibu wa kuuza nyumba umeanza.
Ameeleza kuwa vigezo vya kupata nyumba lazima uwe mtumishi wa umma pamoja na kuwa mwanachama wa Mifuko wa Jamii.
Mkurugenzi wa Ushauri na Ubunifu – WHI Arch. Sephania Solomon, amesema kuwa mradi huo utajengwa kisasa ambapo utakuwa wa ghorofa 12 pamoja na mazingira unaoendana na masisha ya sasa.
Amesema utakuwa na miundombinu ya kisasa ikiwemo mifumo ya kidigitali ili kuhakikisha watumishi wa umma wanaishi katika mazingira rafiki.
Meneja wa Biashara Kampuni ya Shadong Hi- Speed Group Bw. Meng Lingyang , amesema kuwa watahakikisha wanatekeleza mradi kwa ufanisi na kwa wakati.
Watumishi Housing Investnent ni taasisi ya umma ambayo inafanya kazi chini ya Ofisi ya Rais UTUMISHI yenye jukumu la kuendeleza milki na usimamizi wa uwekezaji kupitia uanzishaji na usimamizi wa mifuko ya uwekezaji wa pamoja, WHI kwa sasa inasimamia mifuko miwili ambayo Mfuko wa Nyumba Pamoja na mfuko wa Faida Fund. Mpaka sasa tayari wamejenga nyumba 1, 003 katika mikoa 19 nchini Tanzania.