Mwenyekiti wa Tawi la Simba Igoma Said Mohamed.
Msemaji wa Tawi la Simba Igoma Mwalimu Adi akizungumzia namna wanavyoendelea kufanya amasa.
Basi lililobeba mashabiki wa Timu ya Simba tawi la Igoma.
………….
Na Hellen Mtereko, Mwanza.
Wanachama na mashabiki wa Tawi la Simba Igoma lililopo Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza wamefanya hamasa kuelekea Simba day itakayofanyika Kitaifa Agosti 3, 2024 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Tawi hilo Said Mohamed, amesema wameamua kufanya hamasa kwaajili ya sherehe ambayo itafafanyika kesho Julai 3, 2024 ambayo itaambatana na shughuli mbalimbali ikiwemo usafi.
“Tutafanya usafi kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza pamoja na kuchangia damu nakutoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa waliopo katika kituo cha afya Igoma”, amesema Mohamed
Amesema wanasimba watarajie mambo mazuri kutokana na Timu hiyo kufanya usajili mzuri hususani kwa vijana hivyo watachukua kombe na watarejesha makombe yote ambayo walishayapoteza.
Kwa upande wake Msemaji wa tawi hilo Mwalimu Adi, amesema kila mwaka huwa wanapanda na mwaka huu watapekeka mashabiki wengine sana.
“Tunatarajia kupeleka kosta zaidi ya saba na hadi sasa kosta tano zimeisha jaa, mashabiki wanatamani wafike kwenye tamasha hilo la kihistoria na tunaimani tutaujaza uwanja”, amesema Mwalimu.
Naye Katibu wa tawi la Simba Igoma Asadi Sadiki amesema safari yao ya kwenda Dar es salaam itaanzia kwenye tawi hilo Agosti 1, 2024 sambili asubuhi.