Balozi wa Tanzania nchini Comoro amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ufaransa nchini humo,Sylvain Riquier ikiwa ni ziara ya kujitambulisha.
Balozi Riquier ambaye ni Naibu Amidi wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Comoro amepongeza mahusiano mazuri yaliyopo baina ys Tanzania na Comoro ambazo ni nchi jirani na kutaja kuwa kufanyika kwa Tume ya Ushirikiano wa Pamoja hivi karibuni baina ya Tanzania na Comoro ni hatua nzuri ya kuboresha uhusiano wao.