Leo Jumanne Julai 30, 2024 Tanzania itatupa karata yake ya pili katika mashindano ya Olimpiki ya Paris 2024 wakati muogeleaji Collins Phillip Saliboko, atakapoingia bwawani Saa sita na robo saa za Tanzanis katika Olympic Aquatics Centre kitongoji cha Paris cha St Dennis kushindana katika michuano ya mita 100 (Freestyle) kwa wanaume.
Collins Phillip Saliboko – Kuogelea
*Tarehe ya Kuzaliwa: Aprili 9, 2002
*Mahali pa Kuzaliwa: Mbeya, Tanzania
*Jinsia: Mwanaume
*Uzito: 72 kg
*Urefu: 168 cm
*Kiushindana; Julai 30, 2024 (Saa 6:15 mchana, kwa saa za Tanzania)
Collins Phillip Saliboko ni nyota inayochipukia katika kuogelea nchini Tanzania.
Kijana huyu mzaliwa wa Mbeya, ni muogeleaji aliyeonesha ustadi mkubwa katika bwawa la kuogelea.
Akiwa na urefu wa sentimita 168 na uzito wa kilo 72, Collins ana sifa za kimwili zinazoakisi ujuzi, juhudi na kasi yake awapo majini.
Kujitoa kwake kwenye mchezo wa kuogelea kumemfanya kushiriki katika mashindano mengi ya kimataifa, akiwakilisha Tanzania kwa fahari katika jukumu hilo ngumu kutokana na upimzani mkali sana uliopo katika michezo ya kuogelea.
Collins, ambaye ni bingwa wa Taifa, ameshiriki na kufanya vyema katika mashindano mbalimbali ya kimataifa yafuatayo;
1. Men 50m (Freestyle) World Aquatic Championship Tokyo, Japan, 2023.
2. Men 200m (Butterfly) Commomnwealth Games Birmingham, UK, 2022.
3. Men 50m (Freestyle) CANA Zone IV Swimming Championship 2022, Lusaka, Zambia.
4. Men 200 (Butterfly) 14th CANA African Senior Swimming and Open Water Championship 2021, Accra, Ghana.
NB: Kirefu cha CANA ni Confederation Africaine de Nation (African Swimming Confederation) ambayo sasa inaitwa Africa Aquatics. Ni Shirikisho la bara la Africa linalosimamia michezo yote ya majini. Lilianzishwa mwaka 1970 na wanachama 7. Kufikia mwaka 2008 limekuwa na wanachama 43, Tanzania wakiwa mojawapo.
Tumuombee kijana wetu Collins kila la heri leo.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Mbariki Collins