Na Neema Mtuka
RUKWA
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Mashaka Biteko amewataka wakandarasi wazawa kuacha kufanya kazi kwa mazoea .
Dkt Biteko amesema hayo wakati wa hafla fupi ya uwekaji wa jiwe la msingi la njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovoti 400 kutoka Iringa hadi Sumbawanga na kuunganisha Tanzania na Zambia (TAZA)pamoja na vituo vya kupoza umeme vya Tagamenda, Kisada ,Iganjo Nkangamo na Malangali .
Biteko amesema wapo wakandarasi wazawa wanafanya kazi kwa kusuasua hivyo hana budi kulishughulikia suala hilo na hawezi kulifumbia macho atahakikisha anasimamia ipasavyo ili miradi yote inayoanzishwa kwenye maeneo mbalimbali nchini itekelezwe kwa wakati.
Dkt Biteko Amesema kuwa mradi huo utakapokamili utafungua milango ya kufanya biashara baina ya nchi za jumuia ya kusini mwa Africa SADC na nchi za Afrika ya Mashariki.
Pia amewataka watumishi wa shirika la umeme Tanzania TANESCO kuendelea kufanya kazi kwa weredi na kuzitatua changamoto za umeme pindi zinapotokea .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya Nishati na madini Mathayo Davidi amesema wataendelea kutoa ushirikiano ili kuhakikisha miradi ya nishati inasimamiwa ipasavyo.
Naye mkuu wa mkoa wa Rukwa Makongoro Charles Nyerere ameishukuru serikali kwa kuendelea kuleta maendeleo kwa wananchi na kuongeza kuwa mradi huo utawainua wananchi wa mkoa huo kiuchumi.
Mbunge wa jimbo la sumbawanga mjini Aesh Halfan Hilary amesema moja ya kitega uchumi kikubwa kwa wakazi wa mkoa wa Rukwa ni Nishati ya umeme hivyo amewataka wananchi kuutumia vyema mradi huo kwa manufaa ya sasa na kizazi kijacho.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi akiwemo Annastella Makanji amesema mradi huo utawasaidiakujiimarisha kiuchumi kwani wapo baadhi ya vijana waliopata ajira katika mradi huo.
Mradi huo una urefu wa kilomita 616 kutoka Iringa kupitia kisada Mbeya Tunduma hadi Sumbawanga wenye thamani ya sh Billion 517 ambao utakuwa na faida kubwa kwa mkoa wa Rukwa na nchi jirani.