Ikiwa ni Wiki ya Nenda Kwa Usalama Barabarani Jeshi la Polisi Kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Ngara Mkoa wa Kagera kimeendelea kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya Barabara na kufuata sheria za Usalama Barabarani.
Akitoa Elimu hiyo Leo Julai 29,2024 Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Noel Kagosso ambaye ndiye Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Ngara amewataka madereva wa pikipiki za miguu miwili na mitatu wilayani humo.
ASP Kagosso amewataka kutambua kuwa sheria za usalama barabarani zipo ili zifutwe ili kupunguza ajali zinazoweza kuepukika.
Aidha amewataka kutambua kuwa ajali nyingi zimekuwa zikisababishwa na watu ambao awafuati sheria za usalama Barabarani ambapo amewaomba kuwa mabalozi kwa wengine katika matumizi sahihi ya Barabara ili kupunguza ajali zinazosababishwa na pikipiki wilayani humo.
Kwa upande wake Mkaguzi Kata ya Ngara Mjini Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/INSP Olipa Chitongo amewataka madereva hao kuwa msatari wa mbele kutoa taarifa za watu wanaofanya uhalifu huku akiwaomba kutojihusisha na vitendo vya unyanyasaji katika kata yake.
Vile vile amewataka kutambua kuwa wao wanadhamana kubwa katika sekta ya usafirishaji kitendo kilichopelekea kuitwa maafisa usafirishaji ambapo amesema hategemei kusikia vitendo vya uhalifu vinafanywa na watu wa pikipiki.