AMISHNA Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini,Mzee Ramadhani Nyamka anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara kuanzia Mwaka 1983 hadi 1992(Pichani), Simon Amon Mwanguku kilichotokea leo Alfajiri tarehe 28 Julai, 2024 katika Hospitali Kuu ya Jeshi la Magereza, KMKGM Ukonga, jijini Dares Salaam.
Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Familia linaendelea kuratibu shughuli zote za mazishi ya Marehemu.
Msiba upo nyumbani kwa Marehemu Segerea, migombani, Jijini Dar es Saalam.
Aidha, ratiba ya mazishi itatolewa baada ya taratibu zote kukamilika.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE