Mhe. Jerry William Silaa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
…………….
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaapisha Mawaziri kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam leo tarehe 26 Julai, 2024. Mawaziri hao walioapa ni: Mhe. Jerry William Silaa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Deogratius John Ndejembi kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.
Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mhe. Deogratius John Ndejembi kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.
………………
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pia amewaapisha Manaibu Mawaziri kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam leo tarehe 26 Julai, 2024. Manaibu Mawaziri hao walioapa ni: Mhe. Deus Clement Sangu kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Mhe. Dennis Lazaro Londo kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki). Mhe. Cosato David Chumi kuwa Naibu Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mhe. Deus Clement Sangu kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Mhe. Dennis Lazaro Londo kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki).
Mhe. Cosato David Chumi kuwa Naibu Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki .
Eliakim Chacha Maswi kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria.
Kiseo Yusuf Nowa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro .
Mary Gasper Makondo kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma.
Viongozi Wateule Wakiapa Kiapo cha Maadili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Julai, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali Ikulu Jijini Dar es Salaam mara baada ya tukio la Uapisho tarehe 26 Julai, 2024.