Mkuu wa mkoa wa Rukwa Charles Makongoro Nyerere wakati akizungumza na waandishi wa habari
………………..
NA Neema Mtuka
RUKWA
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere amewataka wafanyabiashara kuendelea kuchangamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza kwenye mkoa wa Rukwa ili kujikwamua kiuchumi.
Makongoro amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa Naibu waziri mkuu na waziri wa nishati Dkt. Dotto Biteko ambapo pamoja na mambo mengine Biteko ataweka jiwe la msingi la mradi wa kusafirisha umeme kilovot 400 kutoka Mkoani Iringa Mbeya hadi Sumbwanga.
Makongoro amesema Dkt Biteko atawasili Mkoani Rukwa kuanzia Tarehe 28 julai 2024 na tarehe 29 ataweka jiwe la msingi la mradi wa kusafirisha umeme .
Amesema Mradi huo una urefu wa kilomita 616 kutoka Iringa kupitia Kisa da Mbeya Tunduma hadi Sumbawanga pamoja na kipande cha kilomita 4 kutoka Tunduma hadi Nakonde mpakani mwa Tanzania na Zambia ili kuunganisha kwa umeme kwa nchi za kusini mwa Afrika pamoja na nchi za Afrika Mashariki.
Aidha Makongoro amesema mradi huo upo eneo la makazi mapya kata ya Malangali Manispaa ya Sumbawanga ambapo Dkt Biteko ataweka jiwe la msingi la mradi huo wenye thamani ya sh Billion 517 ambao utakuwa na faida kubwa kwa mkoa wa Rukwa na Taifa kwa ujumla
Makongoro amesema moja ya faida kubwa ni wananchi kuondokana na changamoto ya kiuchumi hasa wale ambao wanatumia nishati ya umeme katika kujikwamua kiuchumi na kuwataka vijana kuchangamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza kwenye maeneo yao.