Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Godfrey Mnzava amelazimika kukagua Mradi wa Barabara ya Tabora B Nyakati za Usiku unaogharimu kiasi cha shilingi Milioni 253,769,071.75 wilayani Serengeti Mkoani mara ikiwa nijambo la nadra kufanyika katika mbio hizo za Mwenge wa Uhuru
Ujenzi wa Daraja la Tabora B ulianza mwezi mei 2022 na kukamilika mei 4 ikiwa nimpango WA seriki kuboresha miundombinu mbinu ya Barabara kwa fedha za kutoka benk ya Maendeleo ya Ujeruman.KFW Kupitia shirika la hifadhi ya za Tanapa
Mradi huo wa Daraja la Tabora B nikuboresha usafiri kwa wananchi pamoja na mali zao kufika katika huduma za kijamii na masomo kupitia katika miundombinu ya Barabara ambayo ikiwa nisehem ya ujenzi wa madaraja matano kwa mkataba wa jumla ya thamani ya shilingi Bilioni 1147257687.50 Kati ya hizo shilingi Milioni 253 nimetumika katika ujenzi wa Daraja la Tabora B.
Aidha Mradi huo umeleta mafanikio makubwa katika Vijiji vya Bonchugu,Mbilikili,Tabora B bisarara ambavyo Vijiji hivyo havikuwa na miundombinu ya Barabara.