Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Stergomena Tax, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali John Jacob Mkunda Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama Wastaafu Jenerali Robert Mboma na Jenerali Venance Mabeyo ma Meja Godliver Swai Mkuu wa Shule ya Sekondari Makongo wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa jengo la ghorofa la Shule ya Sekondari ya Makongo lililozinduliwa leo Julai 26,2024 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Stergomena Tax, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali John Jacob Mkunda Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama Wastaafu Jenerali Robert Mboma na Jenerali Venance Mabeyo ma Meja Godliver Swai Mkuu wa Shule ya Sekondari Makongo wakifunua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa jengo la ghorofa la Shule ya Sekondari ya Makongo lililozinduliwa leo Julai 26,2024 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Stergomena Tax, akipanda mti wankumbukumbu mara baada ya kuzindua ghorofa hilo katika shule ya sekondari ya Makongo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali John Jacob Mkunda akipanda mti wa kumbukumbu mara baada ya uzinduzi wa jengo hilo.
…………….
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM
Serikali kupitia maboresho ya elimu Tanzania ya mwaka 2023 imejikita kumuwezesha mwanafunzi kupata maarifa, mwelekeo, maadili pamoja na ujuzi ambao utakidhi mahitaji ya Taifa na kumuwezesha katika ushindani wa soko la ajira na kushiriki katika fursa za kiuchumi ndani ya nje ya Nchi.
Akizungumza leo Julai 26, 2024 katika hafla ya Uzinduzi wa Jengo la Madarasa ya ghorofa katika Shule ya Sekondari ya Makongo, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomena Tax,
amesema kuwa katika kumjenga mwanafunzi elimu ya Tanzania itaanzia ngazi awali ili awe na uwezo wa kufikiri na kutafuta fursa.
Dkt.Tax amesema kuwa Shule hiyo itatumika kama kiwanda cha kuzalisha wanafunzi pamoja na kuendelea kujipanga vizuri ili shule iwe ya mfano wa kuigwa.
Dkt.Tax amesema kuwa Shule hiyo inatoa fursa ya kuelimisha jamii na vijana wa kitanzania kwa ujumla ili wajifunze na kutambua uwajibu wao kama watanzania na kuwa na maarifa katika fani mbalimbali na kuchangia katika maendeleo ya nchi.
“Zipo jitihadi zinazofanywa na Shule hii pamoja na Jeshi letu la ulinzi la Tanzania katika kuboresha maendeleo ya elimu nchini na nimeipenda kauli mbiu yao isemayo: Elimu ni Ulinzi” amesema Dkt. Tax.
Ameipongeza juhudi zinazofanywa na uongozi wa shule katika kuhakikisha wanafunzi wanakuwa na maadili mema pamoja na nidhamu, huku akisisitiza umuhimu wa Shule nyingine kuiga mazuri katika Shule hiyo.
Amefafanua kuwa matarajio ya serikali ni kuona elimu inayotolewa nchini ina muwezesha mwanafunzi kujitegemea na kumpatia kipato kutokana na maarifa aliyopata Shuleni.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali John Jacob Mkunda, amesema kuwa lengo ni kuhakikisha Shule za Jeshi zinatoa mchango mkubwa katika sekta ya elimu nchini.
Jenerali Mkunda amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuhakikisha wanatoa elimu bora kwa wananchi wa Tanzania ikiwemo nidhamu bora kwa vijana wanaosoma shule za jeshi.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Stergomena Tax, akizungumza katika uzinduzi huo.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali John Jacob Mkunda akitoa hotuba yake ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomena Tax
Meja Godliver Swai Mkuu wa shule ya sekondari ya Makongo akizungumza katika uzinduzi huo.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Stergomena Tax, akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Majeshi Jenerali John Jacob Mkunda na wakuu wa vyombo vya ulinzi wastaafu Jenerali Robert Mboma. Na Jenerali Venance Mabeyo pamoja na Meja Godliver Swai Mkuu wa Shule ya sekondari ya Makongo.
Muonekano wa jengo hilo jipya ka ghorofa katika shule ya sekondari ya Makongo.