Divisheni ya Uratibu na Ushauri wa Kisheria imeratibu na kuendesha mafunzo ya kitaaluma kwa Mawakili wa Serikali, mafunzo hayo yamefanyika tarehe 26 Julai 2024, katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu zilizoko Mtumba Jijini Dodoma.
Mada kuu katika mafunzo hayo ilihusu Uandishi wa Ushauri wa Kisheria, ambapo mada hiyo iliwasilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi Bw. Ladislaus Komanya aliyeshirikia na Wakili wa Serikali Mkuu Bi Grace Komba.
Huu ni mwendelezo wa utoaji wa mafunzo ya kitaaluma kwa Mawakili wa Serikali unaofanywa na Divisheni ya Uratibu na Ushauri ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambapo hivi karibuni Divisheni hiyo iliendesha mafunzo kuhusiana na ushirikiano kikanda.