Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Suleiman Serera amelipongeza Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kuendelea kufanya uwekezaji mkubwa wa miundombinu ya michezo hapa nchini akitoa wito kwa vyama na mashirikisho mengine vijifunze kwa TFF.
Dkt. Serera ametoa Pongezi hizo alipotembelea kituo cha michezo cha Shirikisho la mpira wa Miguu TFF Kigamboni Jijini Dar Es Salaam leo Julai 17, 2024
Dkt. Serera amesema kuwa serikali inafurahishwa na mwenendo wa shirikisho hilo akibainisha kuwa uwekezaji huo na mipango mizuri inayoendelea kutekelezwa inaongeza ukuaji wa mchezo wa soka hapa nchini.
Kwa upande wake Katibu mkuu wa shirikisho hilo Kidao Wilfred amesema kuwa maendeleo hayo yanatokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya serikali na shirikisho hilo