Benki ya maendeleo Plc imeweka historia ya kuwa benki yenye faida kwa miaka 9 mfululizo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2015 ambapo kwa mwaka 2023 imepata faida ya shilingi Bilioni 2.35 na gawio lake kwa asilimia 50 ikiwa ni shilingi Bilioni 1.17 sawa na shilingi 44 kwa kila hisa.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Peter Tarimo wakati akizungumza na waandishi wa Habari leo Julai 24, 2024 jijini Dar es salaama kuhusu gawio kwa wanahisa kwa mwaka 2024 kutokana na faida ya mwaka 2023
Tarimo amsema mafanikio hayo makubwa ni pamoja na ukuaji wa faida baada ya kodi kwa asilimia 66 kutoka shilingi za kitanzania biliono 1.4 mwaka 2022 hadi shilingi 2.3 kwa mwakq 2023.
“Kuongezeka kwa Amana za wateja kwa asilimia 15 kutoka shilingi za kutanzania bilioni 78.0 mwaka 2023 hadi shilingi za kitanzania bilioni 90.0 mwaka 2023″amesema Tarimo.
“Kuongezeka kwa mikopo kwa wateja kwa asilimia 21 kutoka shilingi za kitanzania bilioni 61.0 hadi shilingi za kitanzania bilioni 74.0 mwaka 2023.
Ameongeza kuwa benki Kuu ya Tanzania BoT imeruhusu gawio hili kutolewa na katika mkutano mkuu wa wanahisa uliofanyika tarehe 22 june 2024 ulipendekeza gawio hilo liwe kwa mfumo wa hisa badala ya fedha tasilimu, hivyo kila mwanahisa atapewa hisa za ziada kwa thamani halisi ya gawio analo stahili kupewa.
Pia amesema Benki ya maendeleo imepata kibali rasmi cha kupanda hadhi na kuwa benki inayofanyakazi nchi nzima ikiwa pamoja na kufungua matawi nje ya Dae es salaam.
“Mafinikio haya yalisubiriwa kwa hamu kubwa kwa miaka mingi kutokana na kigezo cha mtaji ambapo benki ilikuwa na hadhi ya kikanda” amesema Tarimo
Aidha amesema Maendeleo Benki imeendelea kuwekeza kwenye teknolojiq na sasa wapo kwenye hatua za mwisho katika kuanzisha huduma mpya za kidigitali benki ya mtandao(Internet Banking), mfumo wa ukusanyaji wa malipo ikiwemo ada za shule na mikopo kwa njia ya simu.
Kwa upande wake Meneja Usajili wa Hisa na Hati fungani kutoka CSDR, Gideon Kapange amesema hisa zinaanza kuuzwa kwa siku 14 mtu akishanunua hisa za maendeleo bank katika kipindi hiki atastahili kulipwa lile gawio linalotewa kutokana na mahesabu ya mwaka yaliyoishia desema mwama 2023
Pia kuanzia tarehe 14 Agosti 2024 hisa zitaanza kuuzwa bila gawio mpaka katika kipindi kinachoendelea huku daftari la wanahisa likifungwa tarehe 6 Agosti 2024.
Wanahisa wote wanaostahili kupata hawio wale ambao hawajaboresha kumbukumbu zao kwenye daftari la wanahisa wanatakiwa kuboresha kumbukumbu zao kwa kuwapatia namba zao za simu, bank account ili waweze kupata gawio kwa urahisi zaidi.