Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Kinondoni Kusini Mhandisi Florence Mwakasege akizungumza jambo leo Julai 23, 2024, Dar es Salaam wakati akitoa elimu kwa wateja wa Magomeni Kota kuhusu kufanya maboresho ya mfumo wa mita za Luku.
Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Kinondoni Kusini wakitoa elimu kwa wateja wa Magomeni Kota kuhusu kufanya maboresho ya mfumo wa mita za Luku.
…….
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Kinondoni Kusini limeendelea na zoezi la kuwaelimisha na kuhamasisha wateja wake kuhusu kufanya maboresho ya mfumo wa mita za Luku ambao umeaza kufanya maboresho kuanzia Julai 22, 2024 ikiwa na lengo la kuendana na mabadiliko ya mfumo wa mita za luku ya Kimataifa pamoja na kuongeza ufanisi na usalama.
Akizungumza leo Julai 23, 2024 wakati akitoa elimu ya maboresho ya mfumo wa Luku kwa wateja wa Magomeni Kota, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Kinondoni Kusini Mhandisi Florence Mwakasege, amesema kuwa wanaendelea na zoezi la kuwaelimisha wateja katika maeneo mbalimbali katika Mkoa huo ili kuhakikisha wanafanya mabadiliko ya mfumo wa luku kwa wakati.
Mhandisi Mwakasege amesema kuwa lengo ni kuwasaidia wateja kuweza kufanya maboresho kwenye mita zao kwani tunataka wateja wetu wasipata shida wakati wananunua umeme na kuingiza katika mita zao.
Amesema kuwa mteja atakaponunua umeme kwa mara ya kwanza na atapokea tokeni zenye tarakimu za makundi matatu ambapo kila kundi litakuwa na tarakimu 20.
Amesema kuwa kundi la kwanza na pili la tarakimu litakuwa kwa ajili ya maboresho ya mfumo wa luku, huku kundi la tatu kwa ajili ya umeme utakaokuwa umenunuliwa na mteja.
“Mteja ataingiza umeme tarakimu za kila kundi katika luku yake kwa mfatano unaosomeka kwenye risiti ya malipo au ujumbe mfupi wa maandishi (sms) na kila utakapoingiza kundi moja mteja anapaswa kubonyeza alama ya kukubali ya # au msale wa kukubali na hapo utakuwa umefanikiwa kuboresha mita yako na kupokea kiwango cha umeme ulionunua” amesema Mhandisi Mwakasege.
Mhandisi Mwakasege amewataka wateja wa mkoa huo kupiga simu namba 0756 251 753 kwa ajili ya kupata msaada pale inapotokea tatizo wakati wa kufanya maboresho.
Nao wateja wakiwemo Amina Ally pamoja na Nduguru John wamepongeza huduma bora inayotolewa na TANESCO Mkoa wa Kinondoni Kusini ikiwemo kufika eneo la tukio kwa ajili ya kuwasaidia kufanya maboresho ya mfumo wa luku pamoja na kutoa elimu