Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Selemani Said Jafo amefanya ziara ya utembelea shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu kuteuliwa katika Wizara hiyo tarehe 2 Julai 2024
Mhe.Dr.Jaffo ametoa maagizo ya kukamilika kwa mfumo wa ukusanyaji na utambuzi wa fursa za Viwanda nchini unaosimamiwa na TIRDO chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara katika mwaka huu wa fedha kabla ya kufika Juni 2025 ili taarifa hizo ziweze kuleta manufaa kwa sekta ya Viwanda na taifa kwa ujumla.
Awali akitoa taarifa ya Shirika , kaimu Mkurugenzi wa TIRDO Mha. Ramson Mwilangali alimueleza Mhe.Waziri kuwa shirika linaendeleza na kufanya tafiti mbali mbali katika sekta ya Viwanda nchini ili kuibua fursa nchini.
Mha.Ramson alizitaja baadhi ya Kukamilisha Mfumo wa kanzidata ya taarifa za viwanda nchini (National Industrial Information Management System – (NIIMS), Kufanya Tathmini ya Viwanda katika Kanda ya Ziwa na Kuainisha Fursa za Uwekezaji,Kuanzisha Maabara ya Nishati na Madini Mkoa wa Njombe na Ludewa na Kutoa Elimu ya Utengenezaji na Matumizi ya Nishati Mbadala (Safi)
Miradi mingine ni Kukamilisha Ujenzi wa Jengo la Utawala ili Kutoa Nafasi ya Kuanza Kituo cha Taarifa za Viwanda (NIIMS) na Ubashiri wa Teknolojia na Viatamizi kwa Wabunifu wa Teknolojia Katika Shirika Pamoja na Kubadili ithibati ya maabara ya microbiology ya chakula kutoka bodi SANAS kwenda Bodi ya ithibati ya SADCAS.
Baada ya maelezo ya Kaimu Mkurugenziwa TIRDO Mhe.Waziri aliendelea kusisitiza ukamilishajiwa taarifa za Viwanda ‘Mhe.Naibu Katibu Mkuu , nimemsiskiliza Kaimu Mkurugenzi lakini wito wangu ni ukamilishaji wa mfumo huu katika mwaka huu wa fedha, fanyeni mtakavyofanya lakini ifikapo Juni 2025 huu mradi uwe umekamilika’’ alisisitiza Mhe.Jafo.
Katika ziara hiyo Mhe.Waziri aliambata watumishi wengine wa Wizara wakiingozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhe Balozi Dkt .John Stephen Simbachawene ambaye alimhakikishia Mhe.Waziri kuwa maagizo yake yatatekelezwa na kufanyiwa kazi kwa wakati.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TIRDO Mha. Bashiri Juma Mrindoko alimshukuru Mhe.Waziri kwa ziara hiyo na kumhakikishia kuwa bodi yake itashirikiana na menejiment kwa ukaribu ili kufikia malengo ya shirika na kusimamia maagizo yote ya Serikali.