Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 22 Julai, 2024 ametembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini India zilizopo katika Jiji la New Delhi na kupokewa na mwenyeji wake Balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. Anisa Mbega.
Wakati huohuo, Dkt. Tulia amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa tawi la Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini India.