Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa maendeleo ya mpira wa miguu
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda (mwenye miwani) akiwa na viongozi mbalimbali wa Timu ya Pamba Jiji katika mkutano wa wadau wa maendeleo wa mpira wa miguu ulioambatana na uzinduzi wa tiketi za kuingilia kwenye tamasha la Pamba Day.
Wadau wa maendeleo ya mpira wa miguu wakiwa kwenye mkutano katika uwanja wa michezo wa Nyamagana Jijini Mwanza.
……………..
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Kuelekea kwenye tamasha la Pamba Day litakalofanyika Agosti 10, 2024 katika uwanja wa CCM kirumba Timu ya Pamba Jiji imezindua uuzaji wa tiketi za kuingilia kwenye tamasha hilo.
Uzinduzi huo umefanyika leo Julai 22, 2024 katika uwanja wa michezo wa Nyamagana Jijini Mwanza.
Akizungumza kabla ya uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda amewataka mashabiki na wapenzi wa Timu ya Pamba Jiji kujitokeza kwa wingi kwaajili ya kununua tiketi ili waweze kushiriki kwenye tamasha hilo la kihistoria.
Mtanda ameeleza kuwa wanaoweza kuisaidia Timu ya Pamba Jiji isishuke daraja ni wana Mwanza wenyewe hivyo amewaomba kutoa ushirikiano kwa timu hiyo hatua itakayosaidia kuendelea kufanya vizuri zaidi.
“kunatabia ya baadhi ya wadau wa michezo zinapokuja timu zingine zinapokelewa na kupewa siri ya kambi ya timu yetu ili ifanye vibaya kwasababu wanaamini timu ikifanya vizuri na hakuna migogoro maisha yao ya soka yatakuwa hatarini, kwahiyo wanatamani migogoro itokee ili watumie nafasi hiyo kujinufaisha wao jambo ambalo siyo zuri katika ustawi wa tiimu yetu”, amesema Mtanda
Kwaupande wake Mjumbe wa Bodi ya Timu ya Pamba Jiji, Evaristi Agira amesema wanatambua kuwa wako kwenye Ligi kuu hivyo wanatakiwa wacheze mpira kwa juhudi zote ili wazidi kufanya vizuri zaidi.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mh.Stanslaus Mabula amesema jukumu lao la kwanza kama viongozi ni kuhakikisha Timu ya Pamba Jiji inabaki Ligi.