Msemaji na Mwakilishi wa Umoja wa Wahandisi na Wakandarasi nchini Yuda Kemincha akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakieleza adhma yao kutoa mchango wa shilingi Bilioni 10 ili kununua helkopta pamoja na mchango wa mafuta ya shilingi Milioni 100,kwaajili ya kuwezesha shughuli za uchaguzi Mkuu 2025
………………….
NA MUSSA KHALID
Umoja wa Wahandisi na Wakandarasi nchini umeazimia kumnunilia helikopta Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama sehemu ya mchango wao ili aweze kutekeleza shughuli za uchaguzi mwaka 2025.
Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na Msemaji na Mwakilishi wa Umoja huo Yuda Kemincha ambapo amesema hiyo imetokana na kuwa wao ni wanufaika wakubwa wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali yake.
Kemincha amesema kuwa Umoja wa Wahandisi na Wakandarasi wameamua kutoa zawadi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa mchango wa shilingi Bilioni 10 ili kununua helkopta pamoja na mchango wa mafuta ya shilingi Milioni 100,kwaajili ya kuwezesha shughuli za uchaguzi Mkuu 2025
Aidha amesema kama wahandisi na wakandarasi wameguswa na kazi zinazofanywa na Rais Samia ndiyo maana wameamua kumnunulia helkopta kama sehemu ya mchango wao ili aweze kutekeleza shughuli za uchaguzi 2025
‘Tumeamua kutoa helikopta hii ili kumtia moyo kwa kuonyesha kwamba sisi wakandarai na wahandisi tumenufaika sana na miradi mikubwa anayoitekeleza na kuwanufaisha watanzania,mfano mradi wa reli Tanzania tumekuwa ni nchi ambayo tumejenga reli ndefu kuliko nchi yeyote Afrika Km 2000 kuanzia Dar es salaam-Morogoro Km 300,Morogoro –Makutupora Dodoma Km 442,kutoka Dodoma -Tabora Km 249,kutoka Tabora Mpaka Kigoma Km 506 na kutoka Tabora-Isaka Km 130 na kutoka Isaka –Mwanza Km 294 kwa hiyo hayo ni mafanikio makubwa kwenye Reli’amesema Kemincha
Amesema kuwa Helkopta hiyo itawasili mwakani ikitokea Australia ambako inatengenezwa na itakabidhiwa Kwa chama Cha mapindizui Mwakani kabla ya uchaguzi Mkuu.
Vilevile amesema kazi zote zinazofanywa ni za kiuhandisi kinadarasi,lakini pia ujenzi wa barabara ambapo sasa kuna takriba Km 2000 ambazo zimekwisha kukamilika na nyingine zinaendelea kujengwa toka Rais achukue Madakara tangu mwaka 2021.
Akitole mfano Dar es salaam Kemincha amesema kuna ujenzi wa Mwendokasi ambapo ukitoka Kivukoni-Boko tayari mkandarasi yupo,Gongolamboto mpaka Gerezani km 23.6 inakaribia kufika mwisho ,lakini pia ya kutoka Mbagala Mpaka Gerezani.
Amesema Wakandarasi na Wahandisi ndiyo wanufaika wakubwa kwenye miradi midogo na Mkubwa inayotekelezwa ikiwemo miradi ya Barabara,Ujenzi wa shule,hospitali,reli na Bandari hivyo ni muhimu kwao kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu Hassan