*Mshindi wa kwanza wa droo ya promosheni ya Ingia B-Mobile utoke na Iphone 15 Pro ya Bank of Africa Tanzania apatikana
Droo ya kwanza ya kampeni ya kuhamasisha matumizi ya huduma za kidigitali kwa wateja ya Bank of Africa Tanzania ijulikanayo kama “ Ingia B-Mobile utoke na iphone 15 Pro” imefanyika jijini Dar es Salaam, chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha ambapo Ebby Shabani Abdallah, amejishindia simu janja ya kisasa aina ya I-phone 15 Pro.
Akiongea wakati wa droo hiyo, Mratibu wa bidhaa na huduma za kidigitali wa Bank of Africa, Fortunas Joachim, alisema kampeni ilianza Juni 10 mwaka huu na itafanyika kwa kipindi cha miezi mitatu ambapo kila mwezi itafanyika droo na washindi watakuwa wanajipatia zawadi ya simu janja ya kisasa aina ya I-phone 15 Pro, kwa kufanya matumizi ya huduma za kidigitali kama kutuma miamala au kutoa fedha kupitia huduma ya mawakala wa benki ijulikanayo kama BOA WAKALA.
“Kampeni hii ni kwa ajili ya kuhamasisha wateja wetu kutumia huduma zetu za kidigitali kupata huduma za kibenki ambazo zimeboreshwa kuendana na mahitaji ya wateja wetu sambamba na kufanikisha mkakati wa benki wa kutoa huduma zake kwa njia ya kidigitali na kufanikisha ajenda ya kujumuisha wananchi katika kupata huduma za kifedha na matumizi ya huduma za benki” alisema Joachim.
Alisema Benki imejipanga kuendelea kutoa huduma bora kuendana na mahitaji ya wateja wake na itaendelea kubuni kampeni za kuhamasisha wateja wake kurahisisha maisha kupitia kupata huduma bora wakati wowote kupitia njia ya kidigitali.
Kwa upande wake,Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Nandi Mwiyombela alisema “kupitia kampeni hii,wateja wetu na wapya wanaotumia huduma za benki mtandao (Mobile Banking) wataingia katika droo iwapo watafanya miamala 10 kwa njia ya kidigitali na kutoa fedha angalau mara moja kutoka BOA WAKALA.