Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza kusitisha kampeni za kuwania muhula wa pili wa na kusema amechukua uamuzi huo ”kwa maslahi ya chama chake na nchi.”
Uamuzi wa Biden kujitoa kwenye mbio za urais huku ikiwa imesalia miezi minne pekee kabla ya Wamarekani kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu.
Kwa wiki kadhaa sasa Biden amekuwa akishinikizwa ajitoe kwenye kinyang’anyiro hicho na wanachama wenzake wa chama cha Democrats baada ya kufanya vibaya kwenye mjadala na mgombea wa chama cha Republican Donald Trump mwishoni wa mwezi Juni.
Katika barua aliyoituma kupitia mitandao yake ya kijamii, Biden amesema imekuwa ni Fahari ya Maisha yake kuhudumu kama rais.
“Japo ilikuwa ni azma yangu kuwania muhula wa pili, naamini itakuwa ni manufaa kwa chama changu na nchi mimi kujiengua na kujielekeza katika kukamilisha majukumu ya Urais kwa kupindi kilichosalia cha muhula wangu.”