Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imetangaza rasmi matokeo ya mitihani ya 28 ya PSPTB iliyofanyika kuanzia 13 Mei hadi 17 Mei, 2024 katika vituo sita vya mitihani Tanzania bara na Visiwani.
Hayo yameelezwa na Bw. Godfred B. Mbanyi Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB wakati akizungumza na waandishi wa habari alipotangaza matokeo hayo katika Kituo cha APC kilichopo Bunju jijini Der es Salaam.
Amesema jumla ya watahiniwa wapatao 1,280 walisajiliwa ili kufanya mitihani hii ambapo watahiniwa 1,197 (93.5%) walifanya mitihani hii ikiwa ni ongezeko la watahiniwa ukilinganisha na msimu uliopita ulikuwa na watahinwa 977.
Ameongeza. Kuwa kati ya watahiniwa 1,280 Jumla ya watahiniwa 551 sawa na 46.0% wamefaulu mitihani yao ambapo watahiniwa 632 sawa na 52.8% watarudia baadhi ya masomo kuanzia somo moja mpaka masomo matatu kutegemeana na masomo idadi ya masomo aliyofeli, na watahiniwa 14 sawa na 1.2% wamefeli masomo yote waliyofanya katika ngazi zao.
Ametanabaisha kuwa katika masomo 39 waliyopimwa watahiniwa,masomo 24 yalifanywa vizuri, 07 yalifanywa kwa wastani na masomo 08 yalikuwa chini ya wastani.
“Kwa ujumla watahiniwa wa kike walifanya vizuri ukilinganisha na watahiniwa wa kiume. Katika ufaulu wa jumla watahiniwa wawili wakike wakiibuka watahiniwa bora katika ngazi za mitihani za Graduate Professional I, na CPSP” Amesema Mbanyi.
Akizungumzia mikakati ya PSPTB kwa siku za mbele amesema wataendelea kuimarisha na kusimamia ubora wa mafunzo yanayotolewa na vituo vya kuwaandaa watahiniwa (Review Centers) Kuendelea kuimarisha mahusiano ya kitaaluma na Taasisi za elimu ya Juu na Kati ili kuongeza ubora na ufaulu katika mitihani ya PSPTB,
Pia ameongeza kuwa watahimiza na kusimamia uanzishwaji na uendeshaji wa mafunzo kwa kutumia fursa ya nyezo za mitandao zilizopo ikiwa ni pamoja na kuendelea kufanya ziara za kimafunzo vyuoni na katika vito vya mafunzo vilivyosajiliwa na PSPTB ili kuhamasisha usomaji wenye tija kwa ajili ya utendaji mzuri katika mitihani ya PSPTB,
“Tutatembelea pia vyuo mbalimbali vinavyofundisha taaluma ya Ununuzi, Ugavi, Usafirishaji , kushiriki maonesho mbalimbali yakiwemo ya kitaaluma na kutoa alelimu ya umuhimu wa kufanya mitihani ya PSPTB” Amemaliza Mbanyi.