Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jafo amezitaka halmashauri zote nchini kuweka mkakati wa kununuaa dawa za viluwiluwi inayozalishwa na Kiwanda cha TBPL kilichopo Kibaha Mkoani Pwani ili kuua mazalia ya mbu jambo ambalo litasaidia kutokomeza ugonjwa wa malaria ambao umekuwa tishio kutokana na watu wengi kupoteza maisha.
Akizungumza Julai 16, 2024 Mkoani Pwani wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya kutembelea kiwanda hicho, Dkt. Jafo amesema kuwa bado kuna changamoto ya ugonjwa wa malaria nchini, huku akieleza kuwa fedha nyingi zimekuwa zikitumika kutibu wagonjwa.
Dkt. Jafo amesema kuwa katika kutokomeza ugonjwa wa malaria serikali imefanya uwekezaji mkubwa wa kujenga kiwanda cha kuzalisha dawa ya ya kuua mazalia ya mbu ambapo miundombinu yake iligharimu shilingi bilioni 52.
“Bado tuna tatizo la malaria kiwanda hiki kipo Tanzania na ni pekee Barani Afrika, lakini bado hatujaona thamani hasa bidhaa ya matumizi ya kinachozalishwa, leo haiwezekani Kenya Angola,Nigeria Mozambique na Zanzibari wanakuja kuchukua dawa hapa kwetu wakatokomeze malaria kwao, lakini sisi tumejikita katika tiba kutumia fedha nyingi kuagiza dawa badala ya kinga ” amesema Waziri Dkt. Jafo.
Dkt. Jafo meliagiza Shirika la Maendeleo (NDC) kufanya kampeni au kipiga debe dawa hiyo kupitia vikundi mbalimbali, mikutano ya Alati ambayo wanakuwepo viongozi wote wa halmashauri zote nchini ili waweze kwenda na ajenda ya kutangaza dawa ya kuua viluwiluwi vya mbu ili kusaidi kutokomeza malaria na kufikia zero kama Zanzibari walivyofanikiwa.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Maendeleo (NDC) Dkt. Nicolaus Shombe, amesema kuwa uwezo wa kiwanda uzalishaji wake ni mzuri na wataalamu wakati wanajengwa kiwanda hicho lengo kuu lilikuwa kuhakikisha wanapambana na malaria hadi ifikapo mwaka 2030 Malaria inakuwa 0.
Amesema serikali iliyokusudiwa kununua dawa hizo, lakini kwa sasa nchi jirani 6 ikiwemo Botswana, Angola,Mozambique, Nigeria, na kwa asasi mbalimbali za kiraia ikiwemo zinazoshughulika na mazingira ya wakimbizi wamekuwa wateja wakubwa.
“Hii bidhaa ni ya kijamii kama ikinyunyiziwa majumbani sehemu ambazo mazalia ya mbu yanakuwepo wanakufa, lakini nyumba nyingine hazijanyunyizia, kumbuka mbu wanahamahama na zoezi halitafanikiwa, hivyo ni vyemaa jitihada zikafanyika ” amesema Dkt. Shombe
Hata hivyo amesema kuwa Kiwanda hiko kinazalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo mbolea za mazao, chanjo za wanyama na dawa za viluwiluwi.
Katika hatua nyingine Waziri Dkt. Jafo amefanya ziara katika viwanda vilivyopo mkoani Pwani, ikiwemo Kongani za viwanda Modern industrial Park, kiwanda cha Sino tan ambapo amefenya mazungumzo na uongozi wa viwanda hivyo na kuahidi kutatua changamoto mbalimbali zilizopo ikiwemo kuzungumza na Shirika la Reli Tanzania (TRC) kujenga kituo cha treni maeneo hayo ya kiwanda cha Sino tan ili kusidia kuwarahisishia usafiri wanaposafirisha bidhaa.