Dar es Salaam, Tanzania – Julai 12, 2024 – Ubongo, shirika linaloongoza barani Afrika katika burudani ya elimu kwa watoto, linajivunia kutangaza uzinduzi wa ziara zake za kikanda nchini Tanzania, zinazojulikana kama; “Ziara ya Kujenga Akili,” kwa ushirikiano na Vodacom Tanzania Foundation na Hope and Healing International. Ziara ya Kujenga Akili inalenga kutoa uzoefu wa kielimu unaovutia na wenye tija kubwa kwa watoto na walezi kote Tanzania.
Ziara hiyo itaanza katika mikoa ya Mara na Arusha tarehe 15 Julai 2024, ikiwaleta moja kwa moja watoto wahusika wa katuni maarufu barani Afrika na vipindi vya burudani, ikiwa ni pamoja na watoto wenye ulemavu. Iliyoandaliwa ili kuhamasisha kujifunza kupitia michezo, ziara hiyo inatoa mchanganyiko wa kipekee wa elimu na burudani.
“Katika Ubongo, tumejizatiti kutoa maudhui ya kielimu yatakayowezesha viongozi wa kizazi kijacho barani Afrika,” alisema Iman Lipumba, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Maendeleo. “Ziara ya Kujenga Akili ni ushahidi wa kujitolea kwetu kufikia watoto katika kila pembe ya nchi ili kuhakikisha wanapata rasilimali na mafanikio.
Basi lenye chapa ya Ubongo litasafiri katika mikoa hiyo, likibeba wahusika wa katuni na waburudishaji kwa ajili ya kufanya maonesho katika shule na vituo vya kijamii.
Vilevile waatashirikisha watoto katika michezo ya kielimu na mashindano huku ziara hiyo ikilenga kujumuisha sherehe za Mwisho wa juma katika kila mkoa ambapo watoto na walezi wao wataweza kushiriki katika shughuli mbalimbali.
Wakati wa sherehe hizi, watoto na walezi watapokea zana maalum zitakazosaidia mchakato wa ujifunzaji.
“Tunafurahi sana kushirikiana na Vodacom Tanzania Foundation na Hope and Healing International katika ziara hii ya kukuza akili. Ushirikiano huu unathibitisha dhamira yetu ya pamoja ya kutoa uzoefu wa kielimu wa hali ya juu kwa watoto na walezi nchini Tanzania.
Kwa nguvu moja tunalenga kukuza kujifunza kupitia michezo, kusaidia familia, na kuwasaidia watoto wote kufikia ndoto zao kikamilifu,” aliongeza Bi. Lipumba.
Pamoja na hayo ziara hiyo itajumuisha maonesho na uhamasishaji wa programu ya Ubongo PlayRoom na jukwaa la e-Fahamu la Vodacom Tanzania Foundation.
Programu ya Ubongo PlayRoom inatoa mazingira salama yasiyo na vikwazo katika kujifunza, ikijumuisha mkusanyiko wa video, sauti, vitabu vya mtandaoni, na michezo.
Imetengenezwa mithili ya duka moja, programu hiyo inakusanya maudhui yote ya awali ya Ubongo katika sehemu moja ili kuhakikisha urahisi wa kusafiri na kupata maarifa.
e-Fahamu inawapa walimu vifaa vya kuboresha na kuchakata masomo yao na inawapa wanafunzi kupata maarifa katika kujifunza, kuwezesha kujifunza binafsi ili kuelewa zaidi mafundisho ya darasani.
Tunayo furaha isiyo na kifani kuunga mkono Ziara ya Kujenga Akili ya Ubongo ya 2024 kama sehemu ya dhamira yetu ya kuboresha ujifunzaji wa watoto nchini Tanzania. Tunaamini, kwa pamoja, tutahakikisha upatikanaji wa elimu bira kwa kila mtoto,” alisema Sandra Oswald, Meneja wa Vodacom Tanzania Foundation.
Kupitia ushirikiano huu, jukwaa la ubunifu la e-Fahamu la Vodacom Foundation litajumuishwa na maudhui ya kuvutia ya kielimu ya Ubongo, kutengeneza mkondoisho wa teknolojia na ubunifu.
“Kama unavyojua, Ubongo Learning hutumia katuni za kielimu kufundisha watoto wa elimu ya awali na kuifanya iwe ya wa kuvutia, na kwa hivyo, tutasaidia kutumia njia hiyo kwa wanafunzi mbalimbali katika sehemu kadhaa za nchi tutakapofanya ziara,” alisema huku akiongeza kuwa maudhui hayo pia yatajumuishwa kwenye vifaa vya Foundation kama tovuti ya e-Fahamu.
“Hope and Healing International ina chachu ya kuhakikisha upatikanaji na ushirikishwaji kwa watoto wenye ulemavu katika ziara ya Ubongo ya Kujenga Akili hadi mwaka 2024. Tumejizatiti kuhakikisha watoto wenye ulemavu nchini wanashiriki kwa uhuru katika programu za burudani, elimu, na kujenga ari ya kujiamini kupitia michezo ya Ubongo!” alisema Kendra-Lee Heney, Mtaalamu wa Maendeleo ya Watoto katika Hope and Healing International.
Ziara ya Kujenga Akili inalenga kuboresha utayari wa kuanza shule, matokeo ya kujifunza, na kuboresha ujifunzaji kupitia michezo kwa watoto na walezi wao.
Kwa kuleta maudhui ya kielimu moja kwa moja katika jamii, Ubongo inaimarisha dhamira yake ya kuandaa kizazi kijacho cha Afrika na misingi ya kielimu, stadi muhimu, na mitazamo chanya ya kubadilisha maisha na kuifanya jamii kuwa bora siku za usoni.
Mwisho