TUME ya ushindani nchi FCC mezitaka kampuni,taasisi za kifedha,wawekezaji na wazalishaji wa bidhaa,pamoja na wafanyabiashara kuungana kuhakikisha wanatokomeza uingizwaji na utengenezaji wa bidhaa bandia nchini jambo litakalosaidia kuchochea ukuaji wa uchumi.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi mkuu ambaye pia ni mkaguzivwa alama za bidhaa FCC William Erio amesema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa kati ya asilimia 2 mpaka 5 ya biashara zinazofanyika duniani zinahusisha bidhaa bandia hivyo ni wajibu wa kila mwanamaendeleo kuhakikisha anakua mstari wa mbele kupinga na kuzuia matumizi ya bidhaa bandia.
Erio ameongeza kuwa bidhaa bandia kwenye biashara inazorotesha uchumi kwani inawafanya wanaofanya biashara ya bidhaa halisi kukosa soko lakini pia wawekezaji kuogopa kuingia kwenye soko kwani wanakosa nguvu ya kumiliki soko,ila kama serikali na wadau wote watashiriki kutokomeza bidhaa hizo bandia itasaidia kukuza soko.
Erio amesema kuwa kati ya asilimia 2.5 na 3.5 ya biashara zinayofanyika ulimwenguni zinahusisha bidhaa bandia ambapo amebainisha baadhi ya madhara ya bidhaa hizo kuwa ni kutopata thamani halisi ya fedha pamoja na madhara mbalimbali ya kiafya kwa watumiaji
“Wiki ya kudhibiti bidhaa bandia duniani , wiki hii inaadhimishwa sehemu zote duniani kati ya mwezi wa 6 na 7 na sababu yake ni kwamba bidhaa bandia zina matatizo mengi lakini katika biashara zinazoendelea sehemu mbalumbali duniani kati ya asilimia 2.5 na 3.5 ya biashara yote inayofanyika duniani inahusisha bidhaa bandia”
Kadhalika Erio amezitaja athari za bidhaa bandia ikiwemo kunadhorotesha biashara, uchumi na kukosena kwa ajira nchini.
“ Bidhaa bandia zina matatizo hata katika maeneo ya kiuchumi kwanza linaathiri ubunifu kwasababu katika kushindana unatakiwa kila kitu uje na kitu kipya, Kuwa na na bidhaa katika uchumi kunadhorotesha biashara kwasababu pamoja na mambo mengine biashara ya bidhaa bandia inafanyika katika mifumo isiyo rasmi haifuati mifumo ya rasmi ya serikali kwahiyo kuna kodi, ubora wake ni wa chini”
Erio amewataka wadau kuendelea kuungana nao katika kuendelea kutoa elimu kuhudu matumizi ya bidhaa feki ili kuendelea kukuza uchumi nchini
Kilele cha maadhimisho hayo yaliyobebwa na Kauli mbiu isemayo “Kudumisha uhalisia kwa kulinda ubunifu kwa maendeleo ya kiuchumi nchini” kinatarajiwa kuwa julai 18 katika ukumbi wa mikutano ya mlimani city jijini dar es salaam ambapo kutaambatana na maonyesho mbalimbali ya wajasiriamali na wamiliki wa viwanda vidogovidogo pamoja na majadiliano ya jopo.
Haya yanakuja ikiwa ni wiki ya maadhimisho kudhibiti bidhaa bandia duniani yanayotarajiwa kuhitimishwa kesho huku yakiwa na kauli mbiu ya Kudumisha uhalisia katika kulinda ubunifu kwa ajili ya maendeleo ya uchumi.