Mhandisi wa umwagiliaji kutoka Tume ya Taifa ya umwagiliaji mkoa wa Ruvuma Lusia Chaula,akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi wa umwagiliaji skimu ya Nambarapi wilayani Tunduru ambapo Serikali imetoa zaidi ya Sh.bilioni 6.3 ili kutekeleza mradi huo,katikati Mkuu wa wilaya ya Tunduru Simon Chacha na kushoto katibu tawala wa wilaya Milongo Sanga.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Simon Chacha,akizungumza na watumishi wa idara ya kilimo kutoka Halmashauri ya wilaya Tunduru,watumishi kutoka Tume ya Taifa ya umwagiliaji na wakandarasi watakaotekeleza mradi wa skimu ya umwagiliaji ya Nambarapi kata ya Masonya wilayani humo.
Diwani wa kata ya Masonya ambaye ni Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Tunduru Said Bwanali akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya utekelezaji wa mradi wa skimu ya umwagiliaji Nambarapi kata ya Masonya unaotekelezwa na Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa gharama ya zaidi ya Sh.bilioni 6.3.
Mhandisi wa Tume ya Taifa ya umwagiliaji mkoa wa Ruvuma Lusia Chaula kulia,akikabidhi mkataba wa ujenzi wa skimu ya umwagiliaji ya Nambarapi kata ya Masonya kwa Mkandarasi atakayetekeleza mradi huo Reuben Nyagawa kutoka Kampuni ya Africentric Company Ltd.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Africentric Company Ltd Reuben Nyagawa iliyopewa dhamana ya kujenga mradi wa skimu ya umwagiliaji ya Nambarapi kata ya Masonya wilayani Tunduru,akizungumza na wakazi wa kijiji cha Nambarapi na viongozi wa wilaya ya Tunduru baada ya kukabidhiwa rasmi mkataba wa kazi hiyo.