NJOMBE, Baada ya kuona kundi kubwa la walimu wamejiingiza kwenye mikopo umiza na kuathiri utekelezaji wa majukumu yao ya ufundishaji ,Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Makambako kwa kushirikiana na benki ya NMB imetoa elimu ya fedha na mikopo kwa njia ya mfumo wa PEPMIS ili kuepusha usumbufu na mikopo
Wakati Wakifungua mafunzo ya mikopo na matumizi ya fedha yalioandaliwa na NMB kwa walimu wa shule za msingi na sekondari ,Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Wakambako Keneth Haule na Hamza Mandwanga wamesema walimu wanapaswa kuachana na tabia ya kuchukua mikopo mitaani na kutumbukia kwenye matatizo makubwa na kuwaondol
Awali meneja mwandamizi NMB Makao Maku Ally Ngingite na Straton Chilongola meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu kusini wamesema baada ya kutambua changamoto zinazoikumba kada ya walimu na wakalazimika kuja na suluhisho la kifurushi cha walimu chenye huduma nyingi za kifedha ikiwemo mikopo kidigitali na kisha Edfonce Mbasha akaeleza manufaa ya mikopo ya kilimo kwa wlaimu.
Baada kutoa elimu ya fedha na mikopo kwa walimu kupitia mfumo wa PEPMIS ,NMB inakusudia kukutana na walimu wengine kutoka mikoa ya Mbeya na Mkasi Katavi ili kuwakomboa kwenye changamoto hiyo.