Na,Joel Maduka,Msalala Shinyanga.
Mbung wa Jimbo la Msalala,Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga,Iddi Kassim Iddi amemtaka mkandarasi anayejenga Buruma na Matinje kuongeza kasi ya ujenzi kabla ya msimu wa mvua kuanza kutokana na barabara hiyo kuwa na uwitaji wa matumizi muhumu kwa wananchi.
Mbunge Iddi ameyasema wakati wa mkutano wa hadhara ambao umefanyika kwenye kijiji na Kata ya Jana , mapema leo ambapo mkutano huo ni mwendelezo wa ziara yake ya kuzungumza na kusikiliza kero za wananchi.
Amesema hakuna sababu ya kucheleweshwa kufunguliwa kwa barabara hiyo kutokana na kwamba tayari imeshatengewa fedha zaidi ya Sh,Milioni 48.ambapo amemtaka Mhandisi wa Halmashauri ya Msalala kuhakikisha anasimamia Barabara hiyo usiku na mchana iweze kukamilika kwa wakati.
“Mhandisi wa Halmashauri yetu aamesema tayari wameanza kuweka Daraja ambalo litaunganisha kati ya Kijiji cha Buruma na Mwatinje nimuombe mkandarasi aongeze kasi zaidi hakuna sababu ya wananchi wetu kuendelea kuteseka” Alisema Iddi Kassim Iddi,Mbunge wa Msalala
Aidha Mbunge Iddi amegusia suala la Maji ambapo amesema tayari Mchakato unaendelea wa kusogeza Maji na kwamba ni vyema kwa Wananchi wakavuta Maji na kutumia hili waweze kupata mapato.
“Tunamshukuru Rais alitupa kiasi Cha zaidi ya Bilion 1 Kwaajili ya Ujenzi wa mradi wa Maji ambao umekamilika katika hili hatuna budi kumshukuru Rais kwani ametusaidia kwa kiasi kikubwa kwa Kata yetu ya Jana Kupata Maji safi na Salama”Alisema Iddi Kassim Iddi.Mbunge Jimbo la Msalala.
Mbunge Iddi amesema anatambua adha kubwa ambayo wanaipata wanafunzi wa Kijiji cha Buruma kwa kutembea umbali mrefu kwaajili ya kufuata elimu na kwamba ni vyema kwa wananchi wakawa mstari wa mbele kuchangia ujenzi wa madarasa huku akihaidi kutoa kiasi cha Milioni 20 za kuanzisha ujenzi wa shule mpya ya Sekondari.
Katika hatua nyingine Mbunge Iddi amewataka vijana kuchangamkia fursa za ufundi stadi pindi chuo cha VETA kinachojengwa kwenye Halmashauri hiyo kitakapokuwa kimekamilika.