WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nnauye anatarajiwa kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa minara ya mawasiliano ya mtandao wa simu katika Mkoa wa Kigoma na wilaya zake.
Mh Nape atakagua mradi huu ambao unatekelezwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ambao ulianzishwa
kwa lengo la kufikisha huduma za mawasiliano vijijini na
mijini kusiko na mvuto wa kibiashara.
Hali ya mawasiliano ya mkoa wa Kigoma ambao Waziri Nape anatembelea miradi na kukagua ujenzi wa minara kwa jumla ambapo minara 47 imejengwa kupitia ruzuku ya UCSAF kwa teknolojia ya 2G, 3G na 4G.
Ruzuku iliyotumika katika ujenzi wa minara hiyo ni shilingi Bilioni 6.3 na Watanzania Wapatao 866,352 wanaendelea kunufaika na huduma ya mawasiliano
Mpaka sasa, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imeingia makubaliano na watoa huduma ili kujenga Minara katika kata 1974 Zenye vijiji 5,111 na Wakazi wapatao 23,865,957 nchini ambapo mradi huu ukikamilika, jumla ya minara 2,185 itajengwa
Mpaka sasa huduma ya mawasiliano imefikiwa wananchi katika kata 1,349 nchini zenye vijiji 3,933 huku
Jumla ya minara 1,481 ikijengwa na kufikisha huduma ya mawasiliano kwa
wananchi wapatao 16,598,614 ambao wanaendelea wananufaika