Na Mwaandishi wetu
Wanaume wameshauriwa kutoa hisia za maumivu wanayoyapata moyoni kwa kulia ili kuweza kujiepusha na magonjwa mbalimbali.
Imeelezwa kuwa wanaume waliowengi huficha hisia za maumivu yao moyoni pasipo kulia kitu ambacho kimetajwa kuwa na athari kubwa katika maisha yao kwani wanaume waliowengi wamepoteza maisha kwasababu ya kuficha hisia za maumivu yao moyoni.
Akizungumza na wanaume kwenye semina kwa akina Baba wilayani Same mchungaji Nahana Mathias mjema amesema amewataka wanaume kutenga muda wa kulia pindi anapokuwa na jambo ambalo limeumiza moyo wake ilikuweza kutoa sumu hiyo mwilini.
Mchungaji Nahana amesema wanawake wamekuwa na desturi ya kulia na kucheka mara kwa mara katika matukio mbalimbali hivyo wao wamekuwa wakitoa hisia zao za maumivu moyoni lakini wanaume waliowengi huficha hisia zao za maumivu moyoni kitu ambacho ni hatari kwa maisha yao.
“Kweli tunaamini tamaduni nyingi na desturi za familia zetu mwanaume haruhusiwi kulia mbele ya watoto ama mbele ya watu lakini hii imekuwa changamoto kubwa kwa wanaume wengi na kwakuficha na kuzuia hisia zao hizi wengi wamepoteza maisha lakini niwaambietu hata Lazaro wakati Bwana Yesu anapitia mateso Lazaro alilia hivyo niwasihi wanaume lieni mnapokutana na maumivu chukua nafasi hata ukiwa nyumbani kwako ingia ndani chumbani lia kutoa sumu mwilini.”
“Alisema mchungaji Nahana “.
Naye mchungaji Dkt.Enock Mlyuka wakati akizungumza kwenye semina hiyo amesema mwanaume kulia ni jambo la kawaida kwani hutoa sumu mwilini ambayo ingeweza kumletea athari kubwa moyoni kama angeendelea kuficha hisia zake moyoni.
Semina hiyo imeandaliwa na kituo cha ushauri elekezi wilayani Same (SAME COUNCILING FOUNDATION) jumla ya wanaume 116 wamepatiwa elimu ya mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukumbushwa wajibu wao na kusimamia maadili bora kwa watoto wao.