Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack amempongeza Mhashamu Askofu wa Jimbo la Lindi Wolfgang Pisa kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania.
Pongezi hizo amezitoa leo Julai15, 2024 ofisini kwake alipotembelewa na Askofu huyo na kuahidi kuendeleza ushirikiano katika kuhakikisha jamii inaishi katika maadili yanayokubalika.
“Nikupongeze sana kwa kupata nafasi hiyo kubwa ya kuwa Rais wa TEC, ninauhakika baraza hilo unakwenda kulitendea haki mwenyezi Mungu akusimamie akuongoze uweze kufanya kazi yako vile ambavyo Mwenyezi Mungu anapenda iwe ” Mhe. Zainab Telack .
Kwa upande wake Mhashamu Wolfgang Pisa amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Lindi namna ambavyo anatoa ushirikiano kwa kanisa .
” Kama kanisa jimbo katoliki la Lindi tunashukuru sana kwa ushirikiano Mkubwa unaotupatia kanisa la Lindi, kwa maana jimbo katoliki la Lindi ” Mhashamu Baba Askofu Wolfgang Pisa.
Aidha, Askofu Wolfgang Pisa ametumia fursa hiyo kumshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ushirikiano ambao anautoa kwa kanisa katoliki .
“Tunaendelea kumshukuru Mhe. Rais kupitia kwako kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya kwa taifa letu lakini kupitia kwako baraza kama baraza basi tutaendelea kuomba ushirikiano wenu katika maana ya serikali ili tuendele kutumiza majuku yetu yanayotuhusu vizuri “