RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuifungua Bustani ya Mnazi Mmoja Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar, iliyoko jirani na Hospitali ya Mnazi Mmoja, ufunguzi huo uliyofanyika leo 15-7-2024, na (kulia kwa Rais) Mwenyekiti wa Kampuni ya Infinity Group Bw. Samuel Saba na ( kushoto kwa Rais) Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mji Mkongwe Zanzibar. Mhandisi.Ali Said Bakari, akitowa maelezo ya mnara ulioko katika bustani ya Mnazi Mmoja Wilaya Mjini Unguja Jijini Zanzibar. unaoonesha masafa ya maeneo mbali mbali ya Unguja yanayoazia katika enao hilo, wakati wa ufunguzi wa bustani hiyo uliyofanyika leo 15-7-2024.(Picha na Ikulu)
BAADHI ya Wageni waalikwa katika ufunguzi wa Bustani ya Mnazi Mmoja Wilaya ya Mjini Unguja jirani na Hospitali ya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi. (hayupo pichani) akizungumza na kuifungua bustani hiyo ufunguzi huo uliofanyika leo 15-7-2024.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitembelea bustani ya Mnazi Mmoja Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar, baada ya kuifungua leo 15-7-2024, akiwa na Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga.(Picha na Ikulu)