Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Camillus Wambura mara baada ya kufungua Jengo la Makao ya Polisi Mkoa wa Katavi lililopo Mpanda tarehe 14 Julai, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati ukiimbwa Wimbo wa Taifa pamoja na ule wa Afrika Mashariki katika viwanja vya Jengo la Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Katavi tarehe 14 Julai, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Camillus Wambura pamoja na viongozi wengine wakati akivuta kitambaa kuashiria ufunguzi wa Jengo la Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Katavi lililopo Mpanda tarehe 14 Julai, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Camillus Wambura pamoja na viongozi wengine wakati akikata utepe kufungua Jengo la Makao ya Polisi Mkoa wa Katavi lililopo Mpanda tarehe 14 Julai, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi, Maafisa wa Jeshi la Polisi pamoja na Wageni mbalimbali mara baada ya kufungua Jengo la Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Katavi tarehe 14 Julai, 2024.
Taswira ya Jengo la Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Katavi mara baada ya kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mpanda Mkoani humo tarehe 14 Julai, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi mara baada ya kukagua ofisi mbalimbali zilizopo kwenye Jengo la Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Katavi tarehe 14 Julai, 2024.