Na Abel Paul,Jeshi la Polisi Dar es Salaam.
Jeshi la Polisi limeiomba Jamii na kuikumbusha kujikitaka katika malezi kwa watoto ili kujenga jamii inayochukia uhalifu na yenye hofu ya Mungu huku Jeshi hilo likiwaomba wananchi kutoa taarifa za uhalifu na ukatili katika Jamii.
Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es salaam katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph Jimbo Kuu katoliki la Dar es salaam na Mkuu wa Polisi Jamii kituo cha Polisi Kati Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Rose Mbaga alipokuwa akitoa Elimu kwa waumini walio hudhuria ibada hiyo leo Julai 14,2023.
ASP Rose ameongeza kuwa Jamii inapaswa kutambua malezi bora kwa watoto yanaleta mfumo bora wa nidhamu, hofu ya Mungu na kuchukia uhalifu huku akiwataka wazazi kujikita katika malezi bora kwa watoto il ikuzifahamu changamoto zinazowakabili watoto.
Aidha amesisitiza kuwa anafahamu zipo changamoto katika familia ambapo ameomba wazazi kuondoa tofauti zao ili kuwajenga watoto katika makuzi bora.Kwa upande Wake Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Sofia Dilunga ambaye ndiye Mkuu wa kituo Polisi kati Jijini Dar es Salaam amewaomba wazazi kutenga muda wa kukaa na watoto na kusikiliza kero na changamoto wanazopitia watoto wao.
Vilevile amewaomba waumini hao kujikita katika udadisi ili kutambua changamoto zinazowakabili watoto wao huku akitumia fursa hiyo kuwaalika wananchi hao kufika katika kituo cha Polisi kati na kuzumgumza pamoja na kutoa changamoto zinazowakabili katika masuala ya usalama na vitendo vya ukatili.
Nae Padri Prosper Kombe aliyeendesha ibada ya misa hiyo amesema kuwa jambo lolote linataka nidhamu huku akiwaomba waumini hao kujikita katika malezi na kujenga nidhamu ndani ya familia.