Na Sophia Kingimali.
MKURUGENZI wa shahada za awali chuo kikuu Dodoma(UDOM) Dkt.Victor Maliale ameishukuru mamlaka ya maendeleo ya biashara TANTRADE na wadau wote waliowawezesha kupata ushindi wa kwanza huku wakiahidi kuendelea kufanya vizuri na kuhakikisha awatoki kwenye namba hiyo katika maonesho yajayo yakiwemo nane nane.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo na Rais wa Serikali ya mapinduzi Zanzibar Dkt Hussein Alli Mwinyi wakati akihitimisha maonesho ya 48 ya biashara amesema tuzo hiyo imetokana na bunifu na tafiti mbalimbali walizofanya.
Amesema tuzo hiyo ni chachu kwao ya kuzidi kujituma na kufanya tafiti nyingi zaidi ambazo zitaenda kuwa tija katika masoko na Taifa kwa ujumla.
“Kwenye maonesho haya sisi tulikuja na tafiti ambazo zinaenda kushiriki moja kwa moja kwenye soko na kwenye tafitk zetu tunazifanya tunatafiti ndani na tunatafiti nje”,Amesema.
Aidha amesema pia wamekuja na tafiti za kisasa sana kwani wamekuj kutatua changamoto zinazoikabili nchi lakini pia wapo kwenye mpango wa kurusha sateliti ambayo itasaidia kwenye mawasalino.
“Tumeonyesha bunifu ambazo zitasaidia katika ulishaji wa samaki Tumetoa huduma pia katika tiba lishe ambapo hiyo kwetu ni chachu ya wao kuweza kisonga mbele.
“Chuo kikuu cha Dodoma hatuki kuona tafiti zinazofanywa na wanafunzi wetu zinaishia kwenye makaratasi sisi tuzichukua na kuzifanyia kazi na ndio maana leo tunabidhaa hapa zilizotokana na bunifu zetu”
Akizungumzia mwaka mpya wa masomo amesema wamejiamdaa kupokea wanafunzi ambapo dirisha la udahili unanza Julai 15,2023