Na Sophia Kingimali.
Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mgeni Hassan Juma amesema wanawake wamekuwa mabalozi wa kupinga ukatili wa kijinsia na kuchangamkia fursa za kiuchumi kwani wao ni chachu ya maendeleo nchini.
Hayo ameyasema Leo Julai, 12,2024 Mgeni wakati akifungua Jukwaa la Wanawake Viongozi ambalo ni sehemu ya jukwaa lilioendeshwa wakati wa Maonesho ya 48 ya biashara ya kimataifa ikiwa lengo ni kubadilishana uzoefu.
“Wanawake wanapamba katika uchumi na kushirikiana pamoja ili kuendeleza kizazi cha badae lakini changamoto zinaendelea kuwepo pamoja na hizi changamoto leo tuna wanawake marubani, wakandarasi na sekta nyingi tusikate tamaa,”amesema.
Akizungumzia nafasi za viongozi kwa upande wa wanawake amesema Rais Dk.Samia atahakikisha wanashiriki katikà nafasi za uongozi mbalimbali ikiwemo Ukuu wa Wilaya,Wakuu wa Mikoa,Mahakama na sekta zingine.
Amesema huo ni mfano tosha Serikali kutambua mchango wa wanawake kwenye uongozi na ngazi ya jamii.
“Siku ya wanawake duniani ilinzishwa mwaka 1910 iliidhinishwa na Umoja Wa Mataifa (UN) mwaka 1945 kuwa ni siku ya wanaake duniani lengo kubwa ni kuhamasiaha umuhimu wa mwanamke,”amesema
Pia Naibu Spika wa Bunge amewasifu wanawake wanavyopambana katikà kujiongezea uchumi na kuzalisha bidhaa zenye soko ndani na nje ya nchi.
Aidha amesema makongamano kama hayo yaendelee kufanyika kwa lengo la kuwapatia elimu nzuri vizazi vijavyo.
Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE) Latifa Khamisi amesema kongamano hilo lilikuwa na viongozi mbalimbali ambalo limejadili mada nyingi ikiwemo sifa za kiongozi mwanamke.
Aidha amesema wanawake wanapitia changamoto mbalimbali katikà uongozi lakini hawatakiwi kukata tamaa.
“Maonesho ya mwakani wanatarajia kuendelea kongamano la wanawake kwa lengo la kuwaongezea maarifa katikà uongozi wake,” amesema Latifa.
Ameongeza kuwa maonesho hayo yanatarajia kufungwa Julai, 13 mwaka huu na Mgeni rasmi anatarajiwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk.Hussein Ali Mwinyi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Moro Batiki group,Dk. Herieth Mkahanga amesema amejifunza mwanamke akiwa kiongozi ni lazima ataleta mabadiliko chanya.
“Wanawake wanatakiwa kujiamini na kuondoa mifumo dume ndani ya jamii,”amesema.