Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BoT Bw. Emmanuel Rutuba akifurahia jambo na watoto waliotembelea katika banda la BoT katika Maonesho ya Biashara ya 48 ya kimataifa yaliyomalizika leo kwenye viwanja vya Sabasaba Barabara Kilwa jijini Dar es Salaam
…………
BENKI Kuu ya Tanzania BoT imeanza kutoa elimu juu ya maswala ya fedha na uchumi kwa wanafunzi wa shule za msingi ili waweze kuwa na uelewa wa kutosha wakiwa wadogo.
Meneja Uhusiano wa BoT,Vicky Msina ameyasema hayo leo kwenye maonesho ya 48 ya biashara ya kimataifa yaliyofungwa kwenye viwanja vya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.
Ameongeza kuwa ,wao kama benki kuu huwa wanatoa elimu ya maswala ya fedha na uchumi kwa watu wa kada zote wakiwemo wanasheria ,wanasiasa wachumi na wanafunzi wa vyuo mbalimbali .
“Mpaka sasa hivi tumeshuka na tunatoa kwa watoto wadogo kabisa katika elimu ya msingi tunawajengea uwezo wa kutambua maswala ya fedha na uchumi kwani wao ni Taifa la baadaye na ni walimu wazuri sana .”amesema Vicky.
“Sisi elimu tunayotoa hatutoi tu kwa watu wazima peke yao tunatoa pia kwa watoto,kwani huwa ni mabalozi wazuri sana watakapokaa na wazazi wao ni rahisi kuwaelimisha kwa lugha nyepesi na ni wepesi sana kushika ni rahisi sana kwenda kutoa elimu.hiyo kwa wenzao na akitumwa dukani anakuwa makini kukagua hiyo noti.”amesema .
Amesema kuwa ,wanatoa elimu kwa watoto kwani wanatambua kuwa ni watu muhimu ndiyo maana tunawapa elimu pia kwani wao ni wadau muhimu sana katika jamii na watakuwa mabalozi wazuri sana kwa wenzao.
“Kuna makundi maalumu ambayo yameandaliwa kabisa katika kutoa elimu hiyo kwani katika siku zijazo kutakuwa na mitaala maalumu ya kutoa elimu ya maswala ya uchumi na fedha katika ngazi za chini hadi vyuo vikuu na tayari mazungumzo na wizara ya elimu yalishafanyika “amesema.
Meneja Uhusiano wa BoT,Vicky Msina akitoa maelezo ya namna ya kutambua noti kwa watoto waliotembelea banda hilo kwenye maonesho ya 48 ya biashara ya kimataifa yaliyofungwa kwenye viwanja vya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.