Uongozi wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo,Josephat Meza na Afisa Mtendaji Mkuu Arafat Haji wako nchini Comoro ambapo wamefanya mazungumzo na Gavana wa Benki Kuu ya Comoro,Mhe Dkt. Younoussa Imani kwa maeneo mbali mbali ya ushirikiano.
Uongozi wa Benki hiyo wameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Comoro,Saidi Yakubu na pande hizo mbili zimekubaliana maeneo mbali mbali ya ushirikiano.
Benki ya Watu wa Zanzibar ni miongoni mwa benki zinazotambuliwa na Benki Kuu ya Tanzania kama Benki Kubwa na ndiyo inayoongoza kwa operesheni za kibenki visiwani Zanzibar ikiwa imeanzishwa miaka 58 iliyopita.PBZ ina matawi 35 Nchini kote Tanzania