Wakala wa maji Safi na usafi wa Mazingira Vijijini Ruwasa Wilayani Serengeti Mkoani Mara umesema hali ya utoaji wa huduma ya Maji katika Wilaya hiyo inatarajiwa kupanda hadi kufikia Asilimia 68 % kutoka 64,% ya zamani baada ya kukamilika kazi za ukarabati na ujenzi wa Miradi katika Vijiji 19 wilayani humo.
Kauli hiyo ameitoa Meneja wa Ruwasa Wilayani Serengeti Mkoani Mara Mhadisi Deus Mchele katika kikao cha wadau wa Maji ambapo amesema hadi sasa Wilaya ya Serengeti inavijiji 44 vyenye miradi ya maji kati ya Vijiji vyote 78 vya Halmashauri hiyo ambapo inapelekea kufikia wananchi laki moja sabin na nane mia 600 Kati ya wakazi wote laki 2.97.
Pia katika hatua nyingine Mhadisi Mchele amesema katika mwaka wa fedha wanatarajia kuchimba visima 20 nakukamilisha uchimbaji wa visima katika Vijiji nyamakobiti pamoja na nyabilekela.
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti akizungumza katika Kikao hicho ameagiza kuhakikisha visima vyote vinatambulisa kisha Maji yake kuhakikisha yanatibiwa.
Baadhi ya wenyeviti wa Vijiji wameiomba Ruwasa kuhakikisha wanakamilisha miradi yote ya Nyuma ilikuhakikisha inatoa huduma kwa wananchi.