Na Sophia Kingimali.
MAMLAKA ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli na Gesi Asilia (PURA), imewataka Watanzania na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kushiriki katika duru ya kutangaza maeneo ya uwekezaji wa petroli na gesi nchini.
Aidha, imesema mkoani Mtwara imepata mwekezaji mpya wa uchimbaji wa gesi asilia atakayezalisha futi za ujazo milioni 100 kwa siku.
Mwenyekiti wa Bodi ya PURA, Halfani Halfani, ameyasema hayo leo Julai 11,2024 jijini Dar es Salaam, katika Maonesho ya 48 ya kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere.
Amesema wanatarajia kiwango hicho kuongezeka na kitasaidia upatikanaji wa gesi ya uhakika.
Amesema kwa kipindi kirefu wametegemea gesi ya baharini hivyo waamini gesi hiyo itakuwa mpango madhubuti.
Amesema maeneo ya Songosongo Kilwa na Mnazibay Lindi pia wanazalisha futi za ujazo milioni 250 kwa siku na kiasi kikubwa kinatumiwa kuzalisha umeme.
“Asilimia 50 ye gesi hii inazalishia umeme na kiasi kingine minatumika kwenye matumizi mengine,” amesema Halfani.
Kuhusu majukumu ya PURA amesema ni kumshauri Waziri wa Niashati masuala ya mkondo wa juu wa utafutaji, uzalishaji na usambazaji wa gesi nchini.
Amesema jukumu la pili ni kusimamia ufanisi wa juu wa sekta kuhusu utafutaji gesi ili kujua gharama za utafutaji na wapi.
Ameongeza kuwa pia wana jukumu la kuhakikisha Watanzania wanashiriki kwenye jukumu la utafutaji na uzalishaji wa gesi.
Amesema PURA pia ina jukumu la kutunga sera ndogo za kuhakikisha utendaji kazi unakuwa wa ufaniisi lakini pia wanasimamia uuzaji wa gesi nje ya nchi.
Kuhusu miradi iliyopo amesema wanaongeza wawekezaji kwasababu kwa kipindi kirefu hawakuwa na wawekezaji au maeneo mengi walikuwapo lakini maeneo yamerudishwa serikali.
Amesema sheria ya mafuta inasema wawekezaji watafutwe kwa ushindani hivyo wanafanya mkutano wa kutangaza maeneo ya wawekezaji kuyachagua ili kutaka kuwekeza.