Watu kote ulimwenguni wanaadhimisha Julai 11 kama Siku ya Idadi ya Watu Duniani ,iliyoteuliwa na Umoja wa Mataifa ,Tanzania ni miongoni kati ya Nchi ambazo zinaazimisha siku hii muhimu ikiwa na Jumla ya idadi ya watu wapatao Bilioni 61.7 na ukuwaji wa kila mwaka wa asilimia 3.2 huku Mkoa wa Geita ambao unawakazi milioni 2.9 ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 5.4 ukilinganishwa na wastani wa kitaifa.
Akizungumza wakati wa kongamano la kilelele cha maadhimisho ya siku ya idadi ya watu Duniani,ambapo Kitaifa yamefanyika Mkoani Geita, mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo,Naibu waziri ofisi ya Rais ,Mipango na uwekezaji,Stanslaus Nyongo,amesema hapa nchini bado kuna kuchangamoto ya ongezeko la watu ambao auwendani na kiwango cha kasi ya uchimi.
“Hatuwezi kuwa na sera na mipango mathubuti ya kuleta mipango endelevu na yenye usawa kwa nchi Yetu napenda kutambua juhudi za serikali yetu katika kuhakikisha tunakusanya takwimu bora kwa kuzingatia kwanjia inayozingatia haki na usawa hivyo ni vyema tukaendeleza ushirikiano baina ya serikali watafiti mashirika ya Kiraia na wananchi hili tupate takwimu sahihi kwa maendeleo ya Taifa” Alisema Stanslaus Nyongo.
Aidha Naibu Waziri Nyongo ameongeza kuwa uwepo wa dira ya maendeleo umesaidia kwa kiasi kikubwa kuleta maendeleo ya ununuzi wa ndege ,ujenzi wa madaraja ya kisasa,ujenzi wa Zahanati ,Vituo vya afya na Hospital za Kisasa zilizopo Nchini pamoja na Barabara ambazo zimekuwa na changamoto kwa wananchi.
Mwakilishi Katibu mtendaji kutoka tume ya mipango Nchini , Anjela Shayo amesema Mkoa wa Geita ni moja ya Mkoa ambao unashika nafasi ya tatu katika vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia ambapo Mkoa wa Kwanza ni Mara na wa Pili ni Mwanza.
Kwa upande wake Msaidizi wa Mwakilishi mkazi Kutoka UNFPA ,Dkt Majaliwa Marwa amesema Mkoa wa Geita unashika nafasi 3 baada ya mikoa ya Pwani na Katavi.
Maadhimisho ya siku ya idadi ya watu duniani yameambatana na kauli mbiu isemayo Idadi ya watu kitakwimu ni muhimu kwenye kufanya maamuzi sahihi katika sera na mipango ya maendeleo yenye usawa kwa Wote.