Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omary ameeleza kuwa pamoja na changamoto zingine Serikali imeendelea kulipa stahiki za watumishi wa Mkoa wa Lindi ikiwemo madeni ya Likizo, Mishahara na uhamisho.
“Nimshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani ameendelea kulipa Stahiki na maslahi ya watumishi, kwa mwaka huu Bil 1.19 katika maeneo ya madeni ya Likizo, Mishahara na uhamisho”
Ameyaeleza hayo kufuatia taarifa iliyowasilishwa na katibu wa Chama hicho Bi. Sekela M. Simon kuhusu changamoto za baadhi ya watumishi kudai stahiki zao mbalimbali ikiwemo madeni ya likizo hasa kwa walimu wa shule za Sekondari, Kupanda madarasa na uhamisho .
Aidha , Bi. Zuwena ametumia fursa hiyo kuwataka viongozi wa chama hicho Kuzungumza na walimu juu ya umuhimu wa kuwa na weledi katika kusimamaia miradi ya serikali .
“Mwezi juni pekee Mh. Rais Dkt Smaia Suluhu Hassan ametuletea Bili 23 kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya elimu, hivyo kila mmoja hakikishe anasimamaia vema fedha hizo “
Katika mchanganuao wa fedha hizo kila wilaya imepata fedha za ujenzi wa shule mpya na ngazi ya Mkoa imepata fedha za ujenzi wa shule mpya ya wavulana.
Mwalimu Alban Tamba akishukuru kwaniaba ya wajumbe wa kikao hicho amesema wanawashukuru viongozi wa Mkoa wa Lindi kwa namna wanavyotoa ushirikiano katika kutatua chanagamoto za watumishi hasa walimu.
“ tunaomba utufikishie salaum za shukrani kwa mkuu wa Mkoa hasa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna wanavyotupa ushirikiano sisi walimukatika kutatua chanagmoto zetu “