Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Hasani Kabeke akisitiza jambo kwa waumini wa dini ya Kiislamu (hawapo pichani),leo baada ya matembezi (Zafa) ya kuadhimisha mwaka wa 1446.
Sheikh wa Mkoa wa Mwanza,Alhaji Hasani Kabeke,akizungumza na Waislamu leo katikauwanja wa Nyamagana katika mapokezi ya mwaka mpya wa 1446 Hirjjiria.
Mratibu wa Wanawake wa Kiislamu, Hadija Liganga (wanne kushoto), leo baada ya kukabidhiwa barua ya uteuzi katika nafasi hiyo.
Mwenyekiti wa JUWAKITA Mkoa wa Mwanza na Mkuu wa Mkoa mstaafu, Amina Masenza (kulia), leo akipokea jiko la nishati safi ya kupikia kutoka kwa balozi wa mazingira, Mrisho Mabanzo ‘Mr Tree, katikati ni Zakaria Nzuki ambaye alitoa mitungi hiyo kuunga mkono jitihadaza serikali.
…..
NA BALTAZAR MASHAKA,MWANZA
OFISA Elimu wa Mkoa wa Mwanza,Martin Nkwabi amesema wanahitajika walimu
wanaofundisha watoto masomo ya dini wanaozangatia malezi na makuzi yao watoto ili kuwaepusha na mmmomonyoko wa maadili.
Ametoa kauli hiyo leo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo,Said Mtanda wakati
akifunga shereze za kukaribisha mwaka mpya wa Kiislamu 1446 Hirjiria.
“Mnapo sherehekea mwaka mpya wa 1446 kwanza ni kukaa kutathmini(kuangalia)
mafanikio,dosari na kuyaendeleza yaliyopatikana na mwaka huu mna mpango mzuri wa maendeleo.
maadili miongoni mwa watu,kuisha kwa tatizo hili tutengeneze vipindi vya dini
visifundishwe na wasio na maadili,”amesema.Nkwabi amesema shule nyingi zinachangia kuporomosha utu wa mtu haziwabadilishi
watoto na kuwafanya wakue katika maadili,ili kumaliza tatizo la mmomonyoko wa maadili vipindi vya dini vifundishwe na walimu wanaozingatia makuzi ya watoto
hao,si wale wasio wa maadili.“Mafunzo ya dini yakifundishwa na walimu wanaozingatia makuzi na malezi
ya watoto yatakuwa silaha ya kuondoa tatizo hilo la maadili,hivyo tuone namna
ya kuimarisha elimu ya dini pia makuzi na malezi nyumbani familia zisaidie
kuongeza thamani ya watoto na hili waislamu mnafanya vizuri,”amesema.Ofisa Elimu huyo wa mkoa amesema wazazi walio wengi hawawezi wala kufuatilia mafundisho na masomo ya watoto wao shuleni kubaini kama wanafika shuleni au la, bahati mbaya wanawapeleka shule bila kuwa na malengo mahususi watoto wasome ili wawe madaktari,walimu au wataalamu katika kada tofauti.
“Wazazi wengi hawafuatilii mafundisho ya watoto shuleni kama wanavyofuatilia mashamba kuona mazao yao yana hali gani vinginevyo watapata hasara.Bahati mbaya wanawapeleka shule bila malengo,tukiimarisha ngazi ya watoto tutakuwa na kizazi na taifa la maadili,”amesema.
Nkwambi amewapongeza BAKWATA kwa kujenga watu (waumini) wenye uwezo wa
kutawala mazingira yao ikiwemo elimu ya kutambua saratani ya shingo ya kizazi,fistula, kupanda miti na kuchangia damu.
“Binafsi nisigekuwa na maadili ningefanya kazi ninayoifanya au ningefanya uharibifu.Tusaidieni kutengeneza watoto wenye maadili waje kutusaidia,wazazi baadhi hawachukulii uzito kuwapa elimu watoto,tuwekeze katika elimu ya watoto wetu,”amesema.
Sheikh wa Mkoa wa Mwanza,Alhaji Hasani Kabeke amesema wamejipanga
kufanya maendeleo kwa kujenga vituo vya afya saba mkoani humu,hivyo katika kila
shughuli ya kiislamu kutakuwa na changizo la maendeleo kwa hiari bila kumkwaza
mtu.
Sheikh Kabeke amewataka waislamu wasishsindwe kuchangia maendeleo kwa
kukatishwa tamaa na maneo ya watu wazingatiye kauli mbiu ya BAKWATA Mpango Mzima kwa Maendeleo,BAKWATA Mwanza Jenga Hospitali,Bidhaa Tano BAKWATA Inshaallah Tutajenga Hospitali.
Awali Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Mwanza,Ustaadhi Ramadhan Chanila amesema mpango wa miaka mitano wa maendeleo una vipaumbele sita vya kila msikiti kuchangia sh.5000 kwa mwezi,Baraza la Maulid,viwanja na misikiti itakayofanyika shughuli ya kiislamu asilimia 20 itachangia maendeleo huku Ahlul Khayr (Watu wenye Heri) 10,000 wakichangia sh. 1000 na kuendelea.
Amesema BAKWATA mkoani humu imeadhimisha mwaka mpya wa 1446 kwa kupanda miti 175,000 ili kutunza mazingira,kutoa elimu ya saratani ya shingo ya kizazi,fistula,kuchangia
damu,kutembelea mradi JUVIKIBA wa ufugaji samaki kwa vizimba na kuendelesha michuano ya kombe la Mutfi 2024.