Wakala wa vipimo WMA imezishauri Halmashauri kuanzisha vituo vya kuuzia mazao kila Halmashauri ambavyo vitasaidia kuondoa changamoto ya vipimo vya shehena au Lumbesa kwa mazao ya wakulima ambapo sasa mazao yao wanaweza kuuzia kwenye vituo hivyo.
Kauli hiyo imetolewa na Lina Msuya Meneja wa Vipimo Mkoa wa Iringa katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa Jijijni Dar es Salaam ambapo amesema uwepo wa vituo hivyo itasaidia kuondoa changamoto ambayo wakulima wamekuwa wakikutana nayo hususani yakupata maeneo salama ya kuuzia mazao yao.
“Kwa maonesho haya ya Sabasaba tulikuwa tunatoa elimu zaidi kwenye mita za maji kwamba wakala wa vipimo tumeingia kwenye uhakiki wa mita za maji pia tunahakiki Mita za umeme kwa kuhakikisha mtumiaji anapata kulingana na matumizi yake”Amesema Lina Msuya.
Katika hatua nyingine Lina aliongeza kuwa wamekuwa wakitoa Elimu juu ya ufunganishaji mazao ya shamba kulingana na Sheria ya vipimo inataka kuzingatia vipimo sahihi ikiwemo mazao yote yanapaswa kufungashwa kwa uzito wa kilo 100.
” Ukikutwa na changamoto ya kutotekeleza sheria ya vipimo utashitakiwa kwakutofata Sheria hiyo ambapo unaweza kupigwa faini kama utakubali umetenda kosa lakini pia utafikishwa mahahamani”Amesema Linah Msuya
Aidha wakulima na wasafirishaji wameaswa kutumia vipimo sahihi kwani kutokufanya hivyo nikukiuka Sheria ya vipimo Sura no 340.