NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini Mwalimu Mwajuma Nyamka amefanya ziara ya kushtukiza katika tawi la Bamba kwa Mwenyekiti wa shina kata ya Kongowe kwa lengo la kuweza kujionea mwenendo mzima wa maandalizi ya kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Nyamka alisema kwamba kwa sasa chama cha mapinduzi kinajipanga kuanzia ngazi mbali mbali ikiwemo za matawi na mashina na lengo kubwa ni kuwatembelea wanachama na kuwahimiza waweze kujiandikisha kwa mfumo mpya wa njia ya kielectoniki ili waweze kushiriki katikauchaguzi huo.
“Nimefanya ziara ya kushtukiza katika tawi la Bamba lililopo katika kata ya Kongowe na nia kubwa ni kuwatembelea wanachama wa ccm pamoja na viongozi wa matawi na shina ili niweze kujionea ni namna gani wameweza kujiandaa katika kuelekea kwenye uchaguzi wa seriakali za mitaa pamoja na kuwahimiza waweze kujiandikisha,”alisema Nyamaka.
Kadhalika Mwenyekiti Nyaamka alisema kwamba katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu wamejipanga vilivyo na lengo lao kubwa ni kushinda kwa kushindo katika mitaa yote hivyo wanachama wanapaswa kuwa na umoja na mshikamano ili kuweza kupata kura nyingi katika uchaguzi huo
Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo alisema kwamba kwa sasa ni lazima mitaa yote kushiriki kikamilifu katika kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na kuwataka kuendelea kushirikiana bega kwa bega na viongozi waliopo madarakani ili waweze kuendelea kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwa ni moja ya utekelezaji wa Ilani kwa vitendo.