Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 09, 2024 amezindua Tawi la Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) mkoani Morogoro, ambalo kwa kiasi kikubwa litasaidia kupunguza adha kwa Wakazi wa Morogoro na wateja wa benki hiyo kusafiri hadi Dodoma, Dar es Salaam au Zanzibar kufuata huduma za kibenki.