***************
Mkurugenzi Mkuu
wa Tume ya nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) Prof. Najat Kassim Mohammed, leo
amefanya ziara katika Taasisi ya Saratani Ocean Road.
Prof. Najat amepata fursa ya kujionea uwekezaji
Mkubwa uliofanywa na serikali ya awamu ya sita zikiwemo Mashine za X-ray, CT
Scan, MRI, pia kuna Mashine za uchunguzi za nyuklia, Gama Camera n.k.
Prof. Najat pia ametembelea Mashine ya PET-CT/Scan
pamoja na kiwanda Cha Cyclotrone na Mashine za Tiba Mionzi za kisasa za Linac.
Aidha Prof. Najat amesema kuwa amejifunza kwamba
Taasisi ya Saratani Ocean Road ni mfano nzuri katika matumizi ya sayansi ya
mionzi kwa kuwa Taasisi hiyo imepiga hatua kutoka matumizi ya kikale na kwenda
matumizi ya kisasa ya mionzi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Saratani Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage amesema ziara ya Prof. Najat Kassim
Mohammed imetokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya TAEC na ORCI kwa muda
mrefu.
Dkt. Mwaiselage amesisitiza kuwa Taasisi ya
Saratani Ocean Road inatoa huduma za kisasa na za kibingwa za uchunguzi na
matibabu ya saratani ambazo baadhi ya nchi za jirani huwezi kuzipata.
Picha Mbalimbali katika ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) Prof. Najat Kassim Mohammed katika Taasisi ya Saratani Ocean Road.
Picha ya pamoja ya Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) Prof. Najat Kassim Mohammed, na baadhi ya watumishi wa Ocean Road alipofanya ziara yake kwenye Taasisi hiyo.