Afisa Masoko na Mawasiliano Mwandamizi kutoka Mfuko wa Dhamana na Uwekezaji, Bw. Rahim Mwanga (Kushoto), akitoa elimu kuhusu huduma na fursa zinazopatikana katika mfuko huo kwa mwananchi alietembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Afisa Mikopo kutoka Mfuko wa SELF Microfinance, Bw. Joackim Gama (Kulia), akiwaelezea baadhi ya wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha, fursa ya mikopo inayotolewa na Mfuko huo, katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Maafisa wa Wizara ya Fedha, wakimsikiliza Mkazi wa Kigamboni, Bw. Balozi Iddi (kulia), akiuliza maswali mbalimbali kuhusu elimu ya fedha, wakati alipotembelea Banda la wizara hiyo, katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Mchumi Mkuu kutoka Idara ya Usimamizi wa Bajeti Wizara ya Fedha, Bw. Boniphace Kirindimo (Kulia), akimwelezea Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini, Prof. Geraldine Rasheli, namna ambavyo uandaaji wa bajeti ya Serikali unavyofanyika, wakati alipotembelea Banda la Wizara, katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Afisa Mwandamizi kutoka Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Mary Mihigo (Kulia) akimwelezea masuala mbalimbali kuhusu Elimu ya Fedha, Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Mhe. Muharami Mkenge, wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Mratibu Mkuu wa Udahili wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), Bw. John Adelhardus, akimweleza Mwananchi kuhusu fursa ya kozi mbalimbali zinazotolewa na Chuo hicho, wakati alipotembelea Banda la wizara ya Fedha, katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.