Mjumbe wa Baraza la UWT Taifa Bi. Roby Samweli amewataka wanawake kuwa makini na vitendo vya ukatili wa kisiasa kuelekea Uchaguzi wa serikali za mitaa 2024.
Roby ametoa kauli hiyo katika baraza la UWT Mkoa wa Mara ambapo aliwataka wanawake kutumia vyema jukwaa la Kitaifa la UWT la kukabiliana na vitendo hivyo pindi watakapoona viashiria vya ukatili wa kisiasa.
” Niwaombe Sana msiende kunyamaza mnapoona mwanamke aliyesimama kugombea ananyanyaswa toeni taarifa kumsaidia”Roby Samweli Mjumbe wa Baraza la UWT Taifa .
Pia alisema kwa sasa matukio ya ukatili yamepungua kutokana na watu kuelewa na wengine kuficha utoaji wa taarifa lakini anaamini kama wanawake wa UWT wakisisitizwa kusimamia watafanikiwa katika kukabiliana na mbinu chafu baina ya watu wasiopenda wanawake kushika nafasi za Uongozi
Katika hatua nyingine Roby amekabidhi vifaa mbalimbali vya Ofisi katika Mkoa wa Mara ambapo Vifaa vilivyo kabidhiwa nipamoja na wino wa Printer mashine,Limu na Vifaa vingine vya kiofisi.